Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 21 March 2015

UDANGANYIFU KATIKA MAPENZI NA KUBADILI OVYO WAPENZI HUWEZA KUKUINGIZA KATIKA MAGONJWA YA ZINAA


Vijana wengi huwa na tabia ya kubadili wapenzi mara kwa mara pamoja na kutokuwa waaminifu kwa wenzi wao jambo ambalo huwaweka katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya zinaa.

Maradhi ya zinaa ni jumla ya magonjwa ya maambukizi zaidi ya 25 ambayo kimsingi husambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia ya kujamiana.


Magonjwa haya ya zinaa yamekuwa yakisababisha madhara makubwa hasa katika nchi zinazoendelea ambazo nyingi ziko barani Afrika.
Marekani ina kiasi kikubwa cha maambukizi kulinganisha na nchi zingine zilizoendele na inakadiliwa kuwa nusu ya Wamarekani wote huambukizwa magonjwa ya zinaa kabla ya kufikia umri wa miaka 35.

Pamoja na kuenea kwa magonjwa ya zinaa, pia uchunguzi unaonesha kuwa watu wengi hawana ufahamu juu ya hatari za maambukizi ya magonjwa hayo, pamoja na kuwa na madhara au kifo kabisa kinachoweza kusababishwa na matokeo ya kutotibu maambukizi.

Magonjwa ya zinaa kama kisonono au klamidia yanaweza yasionyeshe dalili zozote na wakati mwingine huweza kusababisha kuambukizana kati watu walio katika mahusiano ya mapenzi hali kadhalika maambukizi huweza kumfikia mtoto aliyetumboni hii ni kwa wanawake.

Magonjwa haya yanapoachwa bila kutibiwa, yanaweza kusababisha maumivu makali au kumuondolea mwanamke uwezo wa kupata mtoto.

Watu ambao huwa na wapenzi wengi ndio huwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa ya zinaa na wale ambao hufanya matendo ya ngono bila kujikinga na ambao huchangia sindano za kujidunga madawa katika miili yao.

Uchunguzi mbalimbali unaonesha kuwa watu wenye umri kati ya miaka 16 na 24 wapo katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya zinaa kuliko watu wa makamo kwa sababu vijana wana uwezekano wa kuwa na wenzi wengi wa mapenzi kuliko kuwa na mahusiano ya muda mrefu na mwenzi mmoja.

Lakini sababu nyingine ni kwamba vijana huona ugumu kuwaambia wenzi wao kuwa wameambukizwa magonjwa ya zinaa, pia huona aibu au kutokuwa na uwezo wa kutafuta matibabu ya magonjwa haya. Hii inamaamisha kuwa siyo tu kuwa wanaweza kuambukiza ugonjwa kwa vijana wenzao bali pia wana hatari kubwa ya kupata madhara yanayosababishwa na kutotibu ugonjwa kwa muda mrefu.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu yakiwemo haya ya zinaa unawezafika Mandai Herbal Clinic au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  


No comments:

Post a Comment