Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 3 March 2015

UFAHAMU UGONJWA WA POLIO

Polio ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vinavyoingia mwilini kupitia mdomoni kwa njia ya kula chakula au kunywa kinywaji.


Virusi hivyo hupatikana kwenye kinyesi cha binadamu ambacho huwa na virusi vya ugonjwa wa polio ambapo kinyesi hicho kikiingia kwenye maji na yakatumiwa na mtu kwa njia ya kupikia chakula au kunywa huweza kuambukizwa ugonjwa huo.

Takriban asilimia 90 hadi 95 ya wanaoambukizwa ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote, huku asilimia 5 hadi 10 ya watu huonesha dalili hafifu za homa, maumivu ya kichwa, kutapika, kuharisha, mishipa ya shingo kukaza na maumivu katika miguu na mikono.
Hali hiyo hutokana na virusi hivyo vinapofika kwenye tumbo huweza kusafiri hadi kwenye ubongo na uti wa mgongo ambapo mgonjwa huweza kuhisi maumivu ya kichwa, kukakamaa kwa shingo pamoja na maumivu ya miguu na mikono. 

Kwa kawaida mtu huweza kurejea katika hali ya kawaida baada ya wiki moja au mbili, lakini baadhi yao huweza kupata udhaifu wa misuli suala linalosababisha kushindwa kutembea. 

Hata hivyo, ugonjwa huu huwapata zaidi watoto walio chini ya umri wa miaka miwili kuliko wale ambao wameshavuka umri huo.

Ni asilimia ndogo sana ya wanaopatwa pia ugonjwa wa polio kwa bahati nzuri unaweza kuzuilika kwa kupata chanjo hasa kwa watoto wadogo chini ya miaka miwili. 
 Miongoni mwa dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kuumwa na kichwa, shingo kukakamaa mwili na miguu na mikono kuwa na maumivu. Zipo dalili nyingine ambazo hazionekani mara kwa mara ambazo kupelekea baadhi ya viungo 

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kukutana na Dk Abdallah Mandai sasa na ukapata ufumbuzi wa matatizo yako, kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na inaitwa Mandai Herbal Clinic au unaweza kupiga simu namba  0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment