Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 5 March 2015

UGONJWA WA DENGUE WAANZA KURUDI TENA JIJINI DAR ES SALAAMBaada ya mwaka jana mwezi Mei Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Kutangaza hali ya hatari pale ambapo kulitokea mlipuko wa homa ya dengue , imeelezwa kuwa ugonjwa huo umeanza kurudi jijini Dar es Salaam.


Hii ni kufuatia taarifa za kuwapo kwa watu wawili waliobainika kuwa na homa hiyo katika kituo cha afya cha shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Ugonjwa wa Dengue Taifa, Dkt Hassan Lupinda wa Hospitali ya Mwananyamala alithibitisha kuwapo kwa wagonjwa hao na kusema kuwa hata kama hakuna mvua, mbu wanaoeneza dengue wanaweza kuishi na kuzaliana katika maji yaliyotuama.

"Mbu hawa wanaweza kuishi katika maji safi hata ya nyumbani, hivyo kama watazaliana na kuwashambulia watu katika makazi, wanaweza kusababisha maambukizi” alisema.

Mtaalam kutoka wizarani, Dkt Jubilate Bernad alisema katika kipindi cha mvua za masika lazima magonjwa yamlipuko yatokee na hivyo kutahadharisha kuwa wananchi wajihadhari na mazingira hayo.

"Kwa kawaida magonjwa ya mlipuko yanaweza kutokea , kwa mfano sasa hivi kuna wagonjwa wawili wa homa ya dengue wamegundulika, hawa mbu wanaishi zaidi katika maji yaliyotuama” alisema. 


Jinsi ya kujikinga na homa ya ugonjwa wa dengue

-Fukua madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi yanayozunguka mazingira ya makazi.

-Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo. nk.

-Fyeka vichaka vilivyokaribu na makazi ya watu.

-Hakikisha maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama.

-Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara.Kujikinga na kuumwa na mbu 

-Kutumia dawa za kufukuza mbu ‘mosquito repellants’

-Vaa nguo ndefu za kujikinga na mbu

-Tumia vyandarua vyenye viuatilifu (hata kwa wale wanaolala majira ya mchana)

-Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba unayoishi


 Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment