Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Tuesday, 17 March 2015

UGONJWA WA GOITA NA NAMNA YA KUKABILIANA NAO
Neno Goita ni jina linalotumika katika kuliiita tatizo la kuvimba kwa tezi ya thairoidi iliyo katika eneo la shingo.


Kiufasaha ugonjwa huu wa tezi ya thairoidi unaweza pia kutokea bila kuonekana uvimbe katika eneo hilo.

Ugonjwa huu huonekana kuwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume, hasa wale wanawake wasiopata muda wa kutosha wa kupumzikia na kupata utulivu.

Dalili za mwanzo za ugonjwa huu wa goita ni za muda mfupi na huanza kwa kutokea kama mabadiliko madogo ya kihisia na huweza kupita bila kugundulika.

Baadaye mgonjwa huweza kuwa na dalili za kuwa mwenye huzuni, kupoteza uwezo wa kuzingatia na kulia pia mgonjwa mwenye tatizo hili hukwazika kirahisi sana.

Dalili hizo huweza kufuatiwa na hisia za uchovu uliopitiliza na kutetemeka kwa mikono pamoja na  ukosefu wa nguvu za kuweza kutumia misuli ya aina yoyote mwilini, lakini baadhi ya wagonjwa wengine huweza kuwa na macho kuanza kutokeza kwa nje.

Kupungua kwa uzito ni kati ya dalili zinazojitokeza zaidi kwa wale wanaoumwa ugonjwa huu na huweza kudumu mpaka kufikia hatua ambapo mgonjwa anajisikia kuwa mdhaifu kupindukia.

Chanzo kikuu cha ugonjwa huu ni ukosefu wa madini joto katika chakula na kutokea kwa maudhi mengine ya kihisia na kimwili kunaweza kuliongezea tatizo zaidi.

Chanzo kingine cha kuvimba ni pamoja na mazoea ya kula chakula kilichoondolewa uasilia wake na ambacho hakikupikwa , pia ulaji wa kupita kiasi wa vyakula vilivyopitia kiwandani na vilivyoondolewa ladha asilia.

Matibabu ya uvimbe wa tezi ya shingo  yanapaswa kuanza kwa kuusafisha mfumo wote wa damu na kuanzisha matumizi yam lo unaostahili pamoja na utulivu na mapumziko ya kutosha.

Mgonjwa anapaswa apewe mlo unaostahili pamoja na utulivu na mapumziko ya kutosha kwa kuanzia maji ya matunda kama vile matufaa maji apple, zabibu, mananasi na machungwa yanapaswa kunywewa kwa mpishano wa masaa mawili na nusu kwa muda wote wa siku .

Mgonjwa anapaswa kubadili taratibu mlo wake  na kuanza kutumia mlo ulio na virutubisho kamili. Katika utaratibu huo mgonjwa anapswa kula matunda yaliyo katika hali ya upya wake (fresh), yasiyo na muda mrefu tangu yachumwe.

Matunda hayo yanapaswa kuwa matufaa, machungwa , zabibu, mapeasi, na mdalanzi, jamii na karanga zilizo mbichi na glasi ya maziwa yasiyochekechwa kuondolewa mafuta vitumike asubuhi.

Chakula cha mchana kinapaswa kuwa mboga za majani zilizochemshwa au kupikwa bila kuiva sana , supu ya mboga za majani, saladi za mboga mbichi za majani kama vile nyanya, karoti, kabeji.

Mapumziko ni muhimu kwa mgonjwa anapaswa kupata muda wa kutosha wa kupumzika angalau siku nzima kwa kila wiki kwa miezi miwili,
Mazoezi pia ni muhimu kwa mgonjwa hususani dalili za ugonjwa huu zinapoanza kupotea.

Hali kadhalika mgonjwa apatiwe  vyakula vya madini joto kwa wingi vinapaswa kutumika bila kipimo kwa muda wote kwani humsaidia mgonjwa kupona, vyakula hivyo ni kama mboga za majani, vitunguu swaumu, karoti, vitunguu na nyanya, strawberries na mchele usiolowekwa.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.     
  

No comments:

Post a Comment