Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 11 March 2015

UGONJWA WA KASWENDEUgonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya treponema pallidum.


Ugonjwa huu ni moja ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi.

Ugonjwa wa kaswende huambukizwa kwa njia zifuatazo:
1.     Kufanya ngono zembe yaani kujamiana bila kutumia kinga  na mtu aliyeambukizwa kaswende.

2.      Mama aliyepata ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.

3.     Kuambukizwa kupitia michibuko au mipasuko kwenye ngozi wakati wa kujamiana au wakati mwingine pale mtu anapogusana na mtu mwenye kaswende ikiwa wote wawili wana mipasuko kwenye sehemu mbalimbali za ngozi zao.

Hivyo ndivyo namna mtu anavyoweza kuambukizwa, sasa tuangalie baadhi ya dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende 

Dalili ya kwanza ya aina hii ya kaswende ni kutokea kwa kidonda kidogo cha mviringo katika sehemu ambayo bakteria wameingilia na hutokea kati ya siku 10 hadi miezi mitatu (kwa kawaida kuanzia wiki 2 hadi 6) baada ya mtu kupata maambukizi. 

Kidonda hiki kinaweza kutokea kwenye sehemu ya haja kubwa
Kupata vipele kutokea mwili mzima au sehemu mbalimbali za mwili. Pia muathirika huhisi uchovu, kuumwa kichwa, homa, kunyofoka  nywele, vidonda vya koo, kuvimba kwa matezi mwili mzima, maumivu ya mifupa na kupungua uzito.

Dalili nyingine ni kutokwa vidonda vya rangi ya kijivu kwenye sehemu ya haja kubwa na kwenye tupu ya mwanamke, ngozi kuwa na mabaka meusi kwenye mdomo, sehemu za siri na sehemu za haja kubwa, maumivu kwenye mikono na miguu na pia kuvimba jointi za mifupa. 

Hayo ni machache kuhusu ugonjwa wa kaswende, hivyo ni vyema ukajilinda na kuwa makini ili kuepukana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na madhara makubwa katika afya yako.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment