Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 9 March 2015

UTAFITI:MBWA ANAUWEZO WA KUNUSA NA KUBAINI UGONJWA WA SARATANI
Walimwengu wanasema kuwa ukishangaa ya musa basi utayaona ya filauni, hii ni baada ya watafiti huko nchini Marekani kubaini kuwa mbwa anauwezo wa kunusa ugonjwa wa saratani.


Watafiti hao wanasema kuwa mbwa huyo alifanikiwa kunusa ugonjwa wa saratani ya koromeo , yaani thyroid ambayo hapo awali wakaguzi walikuwa hawakuiona.

Mbwa huyo kutoka nchini Ujerumani, ambaye anaitwa Frankie alifundishwa kunusa mikojo ya watu wenye matatizo na wasio na matatizo ya ugonjwa huo.

Taarifa zinaeleza kuwa mbwa huyo aliweza kugundua saratani hiyo mara 30 katika visa 34.

Kutokana na uwezo huo wa mbwa huyo wanasayansi wanadhani kuwa huenda njia hiyo ikawa njia mpya ya kukagua saratani hiyo ya koromeo, ama ‘thyroid.’ Huku wakibainisha kwamba huenda ikayasaidia maeneo tofauti duniani ambayo hayana vifaa vya kuugundua ugonjwa huo.

SOURCE: BBC NEWS

No comments:

Post a Comment