Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 26 March 2015

UWEZO WA MBEGU ZA PAPAI KATIKA KUTIBU MINYOOUgonjwa wa minyoo ni ugonjwa ambao hupatikana sana katika maeneo yenye hali ya usafi duni.


Maambukizi ya ugonjwa huu hutokea kwa njia ya kula chakula kilichoathiriwa na kinyesi chenye mayai ya minyoo aina ya askaris.

Buu wa mnyoo anapototolewa hujichimbia kupitia utumbo mdogo , mtu mwenye minyoo mara nyingi hawezi kuona dalili zozote endapo idadi ya minyoo ni ndogo, hivyo unaweza kutoona dalili za ugonjwa huu licha ya baadhi ya watu huweza kuhisi  homa, kuhara, na matatizo mengine huweza kujitokeza endapo minyoo hiyo itahamia sehemu nyingine za mwili.

Pamoja na kwamba mgonjwa anaweza kubaki bila dalili zozote kwa muda mrefu, kadri mabuu yanavyozidi kusafiri mwilini huweza kusababisha uharibifu wa viungo vya ndani kama vile kuvimba tumbo, kusababisha sumu mwilini na kichomi.

Kuambukizwa na minyoo mingi huweza kusababisha  utapia mlo, na madhara mengine,  hivyo wakati mwingine ni hatari sana.

Pia minyoo huchukua sehemu kubwa ya virutubisho mwilini kutoka kwenya sehemu ya chakula ambacho bado hakijameng'enya vizuri katika utumbo, hali kadhalika kuna ushahidi mdogo kwamba minyoo pia inaweza kutoboa sehemu ya utando wa utumbo na kujilisha damu, lakini hii si kawaida ya chanzo chake ya lishe.

Mtaalam wa tiba asili na Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbal Clinic, Dkt Abdallah Mandai anasema kuwa mbegu za papai ni moja ya tiba nzuri ya minyoo.

Mtaalam huyo anabainisha kuwa, unapokausha mbegu za papai katika kivuli na kisha kusaga hadi ziwe unga laini ni tiba ya minyoo.

Baada ya kusaga mbegu hizo utakuwa ukichukuwa kijiko kimoja cha chai cha unga huo na uchanganye katika glasi moja ya maji ya moto na baada ya maji hayo kupoa kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kula chakula chochote.

Kwa maelekezo zaidi na maelezo unaweza wasiliana nasi kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443 au fika kliniki yetu iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment