Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 5 March 2015

VYAKULA VYENYE PROTINI HUMLINDA MTOTO NA KWASHAKOOKwashakoo ni ugonjwa unaosababishwa na ukosefu wa chakula chenye protini na mara nyingi huwa ni chakula kilichojaa wanga na starch


Ugonjwa huu mara nyingi huwapata zaidi watoto wa umri wa mwaka mmoja hadi mitano hususani mara baada ya mtoto kuacha kunyonya.

Mtoto mwenye ugonjwa huu huwa anaonesha dalili mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudumaa, nywele kubadilika rangi na kuwa laini, rangi ya mwili hukosa damu pamoja na kuharisha mara kwa mara.

Ugonjwa huu ni hatari pia kwani wakati mwingine huweza kusababisha kifo cha mtomto.

Mtaalam wa tiba asili Dk, Abdallah Mandai anasema kuwa mtoto mwenye tatizo hili anapaswa kupatiwa maziwa yaliyotolewa mafuta (skimmed milk powder) kisha kuchanganya na maji safi au kwenye uji wa mahindi na karanga za kusagwa kisha kumpatia mgonjwa.

Pamoja na hayo, mtaalam huyo anasema kuwa pia mtoto mmwenye tatizo hili anaweza kupewa matunda zaidi kama vile maembe, machungwa, parachichi, mgonjwa anaweza kupewa juisi ya matunda yake au kuponda ponda matunda hayokabla y kumpa mtoto.

Hata hivyo,Dk Mandai anasema pamoja na maelezo hayo, lakini ni vizuri mgonjwa akapelekwa hospitali au zahanati kwa ushauri na matibabu ya magonjwwa hayo.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kukutana na Dk Abdallah Mandai sasa na ukapata ufumbuzi wa matatizo yako, kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na inaitwa Mandai Herbal Clinic au unaweza kupiga simu namba  0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment