Tuesday, 10 March 2015

YAFAHAMU HAYA MENGINE MACHACHE KUHUSU PILIPILI HOHO
Pili pili hoho inatajwa kuwa ni moja ya mboga yenye vitamin nyingi, ingawaje wengi wetu huwa utufahamu.


Aidha, pili pili hoho inaelezwa kuwa na ladha ya kipekee, yenye uwezo mkubwa ya kuboresha mifumo mbalimbali mwilini.

Pilipili hoho inauwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili pamoja na kupambana na maradhi ya saratani, moyo huku pia ikisaidia uwezo wa macho kuona vizuri.

Pilipili hoho zikiwa zimekatwa katwa
Miongoni mwa vitamin ambazo hupatikana kutokana na hoho ni pamoja na vitamin A, C.

Vitamini C huusaidia mwili katika kuukinga dhidi ya saratani ya utumbo mpana , magonjwa ya tumbo na pia huuwezesha mwili kupona haraka majeraha. Huku vitamin A yenyewe ikitajwa  kuwa na umuhimu wa kuongeza uwezo wa kuona  wakati wa usiku.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment