Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 16 March 2015

YAFAHAMU HAYA MENGINE YA MUHIMU KUHUSU KAROTI

Karoti ni tunda ambalo huchukuliwa kama tunda la kawaida, lakini ukweli ni kwamba ni mojawapo ya matunda ambayo yana faida nyingi katika mwili wa binadamu.


Unaweza kupata faida za karoti kwa kuitafuna yenyewe kama ilivyo au hata kuisaga na kuitengenezea juisi bado itabaki kuwa na faida ileile ndani ya mwili.
 
Karoti inaelezwa kuwa na madini mengi ya beta carotene ambayo husaidia katika kuongeza vitamin A kwenye mwili wa binadamu.
 
Inaelezwa kwamba juisi ya karoti husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa makovu yaliyosababishwa na majeraha na hivyo kuiacha ngozi ikiwa nzuri na nyororo.

Unapokula karoti mara nyingi zaidi husaidia kuzuia miale ya jua kutua moja kwa moja kwenye ngozi hali inayomnusuru malaji kupatwa na maradhi ya ngozi ikiwemo saratani.

Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Havard umeonesha kuwa, karoti ina uwezo wa kutoa kinga inayoweza kumuepusha mlaji kupata ugonjwa wa kupooza ‘stroke’
 
Mbali na masuala hayo ya urembo pia karoti ni kinga nzuri kwa macho kutokana na uwezo wake wa kumsaidia mlaji kuwa na uwezo wa kuona vizuri. Hivyo kwa wale ambao husumbuliwa na tatizo la kuona vizuri hii ni tiba sahihi zaidi ya tatizo hilo.

Aidha, karoti pia husaidia kupambana na magonjwa ya moyo kwa mlaji, hii ni kwa sababu ina virutubisho vya alphacarotene pamoja na lutein.

Vilevile karoti inaelezwa kuwa kinga inayowezakupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani hususani ya mapafu na matiti.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

No comments:

Post a Comment