Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 16 March 2015

YAFAHAMU MAMBO MUHIMU ALIYOYASEMA MSAJILI WA BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA KUHUSU TAALUMA HIYO

Kaimu Msajili wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Mboni Zuwena Bakari, amewataka Watanzania  kuzingatia wanapohitaji huduma za tiba asili kwa kufika katika  vituo ambavyo vimesajiliwa na kutambulika na serikali


Akizungumza na kitengo cha Habari kutoka Mandai Herbal Clinic, Mboni alisema kuwa “tiba asili na tiba mbadala ni nzuri lakini jambo la muhimu la kuzingatia ni kuhakikisha unakwenda kwenye kituo ambacho kimesajiliwa” 

Aidha, Mboni alisema kwamba tiba asili ni nzuri na zipo, hii ni kwa sababu kuna maradhi ambayo hayawezi kutibika kwa tiba za kisasa, lakini huweza kutibika kwa tiba asilia.
Kaimu Msajili wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Mboni Zuwena Bakari

“Hizi tiba za asili tulianza kutumia tangu enzi za mababu na watu walikuwa wanapona kikubwa kwa sasa nikuzingatia unakwenda kwenye kituo kilichosajiliwa” alisema Mboni

Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa matabibu matapeli katika tasnia hiyo ya tiba asili, Mboni alisema kuwa, “madkatari feki wapo na ndio maana hata kwenye tiba za kisasa pia kuna madaktari feki, lakini sisi tunachokifanya ni kuhakikisha tunawasajili na wale waliosajiliwa ndio tunawatambua.”

Mandai Herbal Clinic ni moja ya kituo cha tiba asili hapa nchini ambacho kimesajiliwa na kinatabmbulika kisheria na tunatoa huduma za kutibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia mimea na matunda na unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

No comments:

Post a Comment