Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 23 March 2015

YAJUE MADHARA UNAYOWEZA KUYAPATA KWA KUPENDA KUVAA VIATU VIREFU (HIGH HEELS SHOES) MARA KWA MARAViatu virefu ‘mchuchumio’ au viatu vyenye visigino virefu ni miongoni mwa viatu vinavyopendwa na wasichana wengi hapa nchini na hata nje pia.


Wataalam wanaeleza kuwa viatu hivi huweza kusababisha uharibifu wa pingili za uti wa mgongo na huvunjavunja mifupa ya visigino.

Viatu hivi virefu mara nyingi hupendwa zaidi na wasichana wafupi ili angalau na wao waonekane warefu.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa viatu virefu havifai hata kidogo. Kutokana na viatu hivyo kusababisha maumivu makali ya misuli ya miguu pamoja na nyama za nyuma kwenye maungio ya magoti na enka.

Mbali na madhara hayo pia huweza kuchangia uharibifu ndani ya magoti kwa kuhamisha maungio. Kulingana na namna mhusika jinsi anapovaa viatu virefu kwa muda mrefu, ndipo inaposababisha madhara ya muda mrefu pia.

Aidha, huchangia kusababisha mwili kukosa usawa wakati wa kut
embea, kupoteza mwelekeo na mwendo halisi na  misuli ya miguu kubana, huku wakati mwingine huweza kusababisha hata mhusika kuanguka.

Pia viatu virefu husababisha maumivu makali ya kidole gumba cha mguu na hata kuchangia katika kuzuia ukuaji wa kucha pia.

Inapendekezwa kuvaa viatu virefu kuwe kwa muda maalumu kwa shughuli maalumu na viatu husika visizidi urefu wa inchi mbili.

Baada ya kuyafahamu hayo machache ni vyema sasa ukazingatia afya yako wewe mwanamke au msichana kwani kumbuka kuwa pamoja na kutaka urembo, lazima ujali afya yako jambo zuri zaidi ni kuangalia madhara kwa baadaye kuliko kukimbilia kuvaa viatu virefu kwa ajili ya urembo.


Kuwa karibu nasi kwa kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic- mhc na utakuwa ukipata taarifa mbalimbali hususani za afya na tiba asilia kwa ujumla kutoka kwetu Mandai Herbal Clinic. Fanya hivyo sasa, lakini pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa tatizo lolote la kaifya kwa simu namba  0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

No comments:

Post a Comment