Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 13 April 2015

AJALI YA BASI LA NGANGA KUGONGANA NA LORI KISHA KUWAKA MOTO, SABABU YA KUWAKA MOTO HUO IMEBAINISHWAJana kulikuwa na taarifa za kutokea kwa ajali ya basi la Kampuni ya Nganga Express liligongana uso kwa uso na lori  aina ya fuso.


Hata hivyo, jana hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu idadi ya watu waliofariki katika ajali hiyo, lakini taarifa ni kwamba watu 18 wameteketea kwa moto katika ajali hiyo
Magari hayo yaligongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la Iyovi, Milima ya Uduzungwa, mkoani Morogoro. 

Katika ajali hiyo iliyotokea abiria 15 waliokuwa kwenye basi na wengine watatu wa lori waliteketea kwa moto huku wengine 10 wakijeruhiwa vibaya. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul amesema  kuwa, ajali hiyo ilitokea baada basi hilo lililokuwa linatoka Kilombero kwenda Mbeya likiwa kwenye mistari ya barabarani ya katazo na kwenye mwendo kasi kugongana na lori lililokuwa limebeba matikiti na kuwaka moto. Alisema majeruhi wanne wamelazwa katika Hospitali ya St. Kizito, Mikumi na sita wako katika Hospitali ya Mtandika, Iringa. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ameongeza kuwa,  kwenye basi hilo kulikuwa na pikipiki ambayo pia iliungua inawezekana ndiyo iliyosababisha moto huo. 

Kutokea kwa ajali hiyo ni mfululizo wa ajali zinazotokea katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania juma hili, ikiwa ni siku moja baada ya watu watano kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mikoa ya Dodoma na Iringa. 

Nchi imekuwa ikishuhudia ajali za mara kwa mara za barabarani ambapo makumi ya watu wamekuwa wakipoteza maisha yao, huku uzembe wa madereva na mwendo wa kasi zikitajwa kuwa sababu kuu zinazosababisha mlolongo wa ajali hizo.


Mandai Herbal Clinic inatoa pole za dhati kwa wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali za hiyo, Mwenyezi Mungu awape nguvu ndugu wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na kuwapa ahueni mapema majeruhi wa ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment