Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 17 April 2015

DK MANDAI LEO ANAKUPA NAFASI YA KUUJUA MMEA HUU UITWAO MLANGMIA WENYE UWEZO WA KUTIBU MAGONJWA MENGIDk Abdallah Mandai

Tumekuwa tukielezea mimea na matunda mbalimbali yanavyoweza kuwa tiba ya magonjwa mbalimbali, kwa huo ndio utamaduni wetu kuendeleakutoa elimu ya mimea tiba kwako


Sasa leo nimekusogezea mmea huu aina ya mlangmia huu ni miongoni mwa ile mimea mingi ambayo ilitumika sana enzi hizo katika kutibu magonjwa mbalimbali.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema, mmea huo ni wa ajabu sana na ni miongoni mwa mmea ambao hauna shina, huku akibainisha kuwa chanzo cha mmea huo ni kiazi, ambapo baada ya kamba huchomoza na kutoka ardhini na kisha kujizinga katika mti na baadaye kiazi na kamba hiyo huachana.

“Mlangamia au mtotokanga ni mti wenye maajabu sana na hauna shina, lakini unasambaa juu ya mti, huku ukiwa umestawi vizuri,” alisema Dk  Mandai.

Aidha, Dk Mandai anaendelea kueleza kwamba si rahisi kiazi cha mmea huo kuchimbwa na mtu wa kawaida labda awe ni mzee au mwenye utaalam kuhusu mambo ya tiba asili.

Anasema mmea  huo unasifika kwa kutibu magonjwa ambayo watu wanasumbuka nayo, lakini wakienda hospitalini kupimwa hayaonekani.

Dk Mandai,  inafafanua kuwa kiazi hicho kinatibu magonjwa ya moyo na hasa moyo uliopanuka, huku akiongeza kusema “kwamba wazeee wetu walitumia sana mmea huu kuondokana na magonjwa ya moyo,” pia anasema wengine walitumia mmea huu kwa watoto wazito wa kutembea, ambapo walikuwa wakiwafunga kamba za mti huu kiunoni na walikuwa wepesi wa kutembea.

“Kwa wale wenye matatizo ya kukohoa kikohozi kikavu kabisa hadi wakati mwingine wanatoa machozi dawa hii huweza kutibu kabisa hadi mtu anapona kabisa,” anaeleza. 

Pia Dk Mandai anaendelea kueleza kuwa dawa hiyo husaidia kwa mtu mwenye tatizo la kukaukiwa sauti, anayesumbuliwa na athma, ambapo anasema ile kamba ikichemshwa na mtu wa tatizo hilo akitumia maji yake anapona.

Mbali na hayo, Dk Mandai anaeleza kuwa mmea huo ni suluhisho la matatizo ya kinamama hususani kwa wale wenye matatizo ya kukosa nguvu wakati wa kujifungua, ambapo anaeleza kuwa mama mwenye matatizo hayo anapochemshiwa kamba za mmea huo kisha akanywa maji yake basi mama huyo atajifunguwa kwa urahisi bila shaka.

Hali kadhalika anaongeza kwamba, kwa mama mwenye changamoto ya kutokuwa na maziwa ya kutosha kumnyonyesha mtoto wake, mmea huo pia ni msaada mkubwa iwapo mama huyo atakunywa maji ya dawa hiyo baada ya kuchemshwa.

Mbali na hayo, unaponya magonjwa mengine sugu kama kusafisha figo na mapafu, ambapo anasisitiza kuwa unatibu magonjwa hayo kutoakana na maajabu ulio nayo.
Karibu Mandai Herbal Clinic ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu au ndugu yako pia unaweza kumleta. Tupo Ukonga, Maongolandege jijini Dar es Salaam pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku  


No comments:

Post a Comment