Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 30 April 2015

EEH! HII NAYO KALI ETI MWANAFUNZI AFUKUZWA SHULE KISA ALIVAA SKETI YA SHULE NDEFU KULIKO ZA WENZAKE!!Wakati shule nyingi hapa nchini zikiwa na utaratibu wa kuwahimiza wanafunzi wa kike kuvaa sketi ndefu wanapokuwa katika mazingira ya shule, huko nchini Ufaransa wao hali ni tofauti.


Ni baada ya msichana mmoja muislamu kukatazwa kuingia darasani kwa sababu alikuwa amevalia sketi ndefu.

Msichana huyo mwenye umri wa 15 alifukuzwa kutoka shuleni hapo na utawala wa shule hiyo uliodai amekiuka sheria za nchi hiyo zinazokataza kuonesha waziwazi ishara za kidini.

Kwa kawaida msichana huyo aitwae Sara, huvua hijabu yake anapokuwa maeneo ya shule kama inavyoamuriwa lakini hakudhani kwamba sketi yake ndefu pia ingemuweka matatani.

Inaelezwa kuwa hiyo ni mara ya pili Mkuu wa shule hiyo amemrudisha nyumbani mshichana huyo baada ya kumpa barua awapelekee wazazi wake inayoagiza kuwa abadilishiwe mavazi ndio aruhusiwe kuingia darasani. 

Inavyoelekea mgongano huu unatokana na tafsiri hiyo ya sheria ya 2004 inayozuia raia wa nchi hiyo kuonesha wazi wazi kuwa ni waumini wa dini fulani.

Msichana Sara yeye anasema sketi yake si vazi la kidini, lakini utawala wa shule unatafrisi sketi hiyo yenye urefu wa hadi juu kidogo tu ya kisigino, kuwa vazi la kiislamu.

Asante kwa kuchagua tovuti hii ya www.dkmandai.com kuwa moja ya sehemu yako ya kupata taarifa mbalimbali, tambua kwamba tunathamini sana uwepo wako mdau wetu, pia unaweza kuwa karibu nasi zaidi kwa kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist  Clinic- mhc na utakuwa ukifikiwa na taarifa zetu zote. Pia kama unatatizo lolote la kiafya wasiliana nasi kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Au Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.
No comments:

Post a Comment