Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 17 April 2015

ENDELEA KUZIFAHAMU SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA UGUMBA KWA WANAWAKEHabari za leo mpendwa msomaji wa tovuti yetu bila shaka utakumbuka jana Aprili 16, 2015, tulizungumzia kuhusu tatizo la ugumba kwa wanawake na tukaeleza sababu kadhaa ambazo huchangia tatizo hilo.


Hivyo leo nimeona tumalizie sababu nyingine ambazo huweza kuchangia tatizo hili la ugumba.

Kuziba kwa Mirija.
 Hii ni moja ya sababu inayoweza kuchangia tatizo hili, kawaida mwanamke ili aweze kupata mtoto ni lazima yai lake liweze kusafirishwa kwenda kwenye mji wa mimba kupitia mirija ya ‘fallopian tube’ na ikitokea ‘fallopian tube’imeziba  au kuharibika, kuna vitu vingi hutokea sababu ule uharibifu unaotokea kwenye ule mrija huweza kusababisha mimba kutungia nje ya kizazi na huweza kuondolewa kwa mrija ambao una hitilafu, hivyo mtu huwezi kupata mimba.

Msongo wa mawazo
Kuwa na msongo wa mawazo pia huweza kuwa chanzo cha tatizo ( emotional stress) husababisha ‘hormone imbalance’ yaani homoni kutokuwa sawa, ambayo husababisha mayai kushindwa kukomaa.

Matumizi ya Kemikali
Matumizi yenye vitu vyenye kemikali nyingi huweza kusababisha homoni kutokuwa sawa na kupelekea shida ya kutokukomaa kwa mayai na kusababisjha ugumba.

Matumizi ya Sigara
Matumizi ya sigara huweza kuchangia tatizo hili la ugumba. Hivyo wanawake hushauriwa kuepuka matumizi ya sigara.

Kizazi kukaa upande
Sababu nyingine ni kugeuka kwa kizazi au kukaa upande pia huweza kuchangia kwa asilimia kubwa mwanamke kushindwa kupata ujauzito.

Kama umekuwa ukisumbuliwa na tatizo hili kwa muda mrefu unaweza kutumia fursa ya kufika Mandai Herbal Clinic kwa uchunguzi zaidi kisha utapata dawa ambazo zitaweza kukusaidia kuondokana na tatizo hilo.

Mandai Herbal Clinic tunapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana nasi kwa namba za simu zifuatazo 
0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku

No comments:

Post a Comment