Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 21 April 2015

FAHAMU NAMNA YA KUJENGA UHUSIANO MZURI KATIKA HISIA ZA WATOTO
Jinsi wazazi wanavyokabiliana na watoto ni muhimu sana katika hisia za mtoto. Uhusiano kati ya mzazi na mtoto huweza kuwa na athari katika hisia za mtoto endapo hautazingatiwa.


Watoto huwa na uwezo wa kukabiliana na hisia kwa kuangalia jinsi watu wa familia wanavyokabiliana na hisisa zao. Mzazi huwa kiungo muhimu sana kwa kumpa mtoto mbinu za kukabiliana na hisia nzito.

Watoto huhitaji usaidizi na mazoezi katika kukabiliana na hisia zao, hivyo leo nimeona ni vyema nikujuze hizi njia kadhaa za kujenga hisia za mtoto.

1.     Weka mazingira ya nyumba kuwa tulivu na yenye kuridhisha.

2.     Kubaliana na hisia za mtoto kwa wakati huu na kuzishughulikia.

3.     Wasomee hadithi watoto, hususani zile zenye hisia, hii inasaidia mtoto kuelewa zaidi kuhusu hisia zake mwenyewe.

4.     Mfundishe mtoto kujieleza kwa kutumia maneno . Mfano, “yaonekana kama huna raha”

5.     Jaribu kujua hali zinazofanya mtoto kuwa na wasiwasi, raha, hasira au hofu.

6.     Kumbuka kumsifia mtoto pindi anapokuwa na tabia njema.

7.     Mfundishe pia mtoto kujua hisia na maadili. Mfano wakati mtoto amehuzunika unaweza kumwambia ‘Hivi sasa najua una huzuni, lakini unafanya ndugu zako kuwa na huzuni zaidi’

Hayo ndio machache kwako mzazi ni vyema ukayazingatia ili kumfanya mtoto kuwa katika maadili mazuri. Iwapo unatatizo lolote la kiafya tafadhali fika Mandai Herbal Clinic, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. No comments:

Post a Comment