Tuesday, 21 April 2015

FAIDA ZA SUPU YA MBOGA ZA MAJANI NA MCHANGANYIKO WAKE
Karoti, pilipili hoho zile nyekundu, nyanya na mboga za kijani kibichi vikitumiwa kwa usahihi huwa ni dawa na kinga ya maradhi yatokanayo na saratani.


Lakini pia vitu hivyo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu na namna ya kutumia vitu hivyo kama tiba ni kama ifuatavyo:

Maelekezo yake ni kwamba, vitu hivyo vilivyotajwa hapo juu unatakiwa kuvichanganya kwa pamoja ambapo utatokea mchanganyiko wa mboga za majani zenye rangi ya kijani kibichi aina tatu hadi tano tofauti.

Unachopaswa ni kuchukuwa kiasi cha kila aina ya mboga , kisha unaosha vizuri na kuzikatakata na kuzichanganya na karoti, nyanya, pilipili hoho na kuzichemsha kwa pamoja kwa muda wa dakika tano hadi kumi na tano.

Baada ya hapo supu itakayopatikana hapo kutokana na mchanganyiko huo huwa tayari kwa kunywewa (matumizi) 

Unaweza kutumia supu hiyo asubuhi au usiku, kwa muda wa wiki moja jitahidi unywe mara tatu na unaweza kuitumia hivyo kwa muda wa mwezi mmoja au zaidi.

Iwapo unatatizo lolote la kiafya tafadhali fika Mandai Herbal Clinic, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. No comments:

Post a Comment