Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 28 April 2015

FURAHA YETU NI KUONA WATOTO WANAKUWA NA AFYA BORA, NDIO MAANA HAPA NIMEKUWEKEA HIZI FAIDA ZA MTOTO KUNYONYAWazazi wengi wa sasa wamekuwa ni wavivu kidogo katika suala la kumnyonyesha watoto kutokana na shughuli na mihangaiko yao ya kila siku ya kutafuta maisha.


Lakini ukweli ni kwamba mtoto kunyonya ni jambo muhimu sana, tukiacha mbali na faida za kiafya za maziwa ya mama kwa mtoto.

Kuna baadhi yao hushindwa kunyonyesha kwa madai ya kuhofia kuharibu shape za miili yao sababu ambayo haina mashiko kabisa kwa mzazi makini na mwenye kumjali na kumpenda mtoto wake.

Leo nakuweka karibu na hizi faida za mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama.

Kwanza maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto, ambayo humsaidia mtoto kumlinda na magonjwa mengi ya utotoni.

Pia kitendo cha mama kukaa kumnyonyesha mtoto wake husaida sana kujenga ukaribu kati ya mama na mtoto.

Kunyonyesha husaidia kupunguzia uwezekano wa mama kupata saratani  ya matiti.


Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 


No comments:

Post a Comment