Wednesday, 22 April 2015

HIVI UNAZIJUA FAIDA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO YENYE LIMAO? NIMEKUWEKEA HAPA
Kuna baadhi ya vinywaji huenda ikawa ni vigumu kwa wengi wetu kupenda kuvitumia au kuvipa kipaumbele kutokana na ladha yake kutokuwa nzuri mdomoni, lakini pengine huwa na manufaa.


Leo kuna hizi faida za kunywa maji ya moto yakiwa yamechanganywa na limao.

Kwanza kabisa maji haya yanuwezo wa kusaidia kuongeza kinga ya mwili na hasa kupambana na magonjwa madogo madogo kama mafua, na kikohozi, hii ni kutokana na kuwa na vitamin C.

Husaidia pia kusafisha mfumo wa chakula na kuondoa sumu mwilini, huku ikisaidia kuzuia tumbo kujaa gesi mara kwa mara.

Kinywaji hiki pia husaidia majeraha kupona kwa haraka kutokana na kuwa na ascorbic acid ya kutosha, lakini pia huimarisha mifupa.

Huimarisha ngozi na kuondoa makunyanzi pamoja na kukupa muonekano mzuri zaidi.
Pia husaidia sana kwa wale wenye uzito mkubwa kupunguza uzito kwani maji ya moto na limao huyeyusha mafuta ya kutosha.

Husaidia kuyapa macho afya nzuri zaidi na kuimarisha kuona vizuri.

Hali kadhalika huondoa uchovu na kukufanya kuwa mchangamfu na kukufanya siku yako ianze vizuri.

Pamoja na hayo yote pia husaidia sana kuleta hewa safi kinywani.

Mandai Herbal Clinic tunatibu magonjwa mengi yakiwemo yale sugu kwa kutumia tiba asilia zitokanazo na matunda na mimea. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam, pia tunapatikana facebook kwa jina la Mandai Herbalist Clinic-mhc ambapo pia unaweza kulike page yetu hiyo na kuuliza maswali yako huko. 

Kwa mawasiliano mengine ni 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 
 

No comments:

Post a Comment