Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 2 April 2015

HIZI HAPA FAIDA NYINGINE ZA MATUMIZI YA ALIZETI


Alizeti ni moja kati ya mazao ambayo hupatikana hapa nchini katika baadhi ya mikoa ikiwemo Singida na Iringa.
Zao la alizeti hutumika hasa kwa kuchuja mafuta yake ambayo hutumika sana kwa kupikia.

Mtaalam wa tiba asilia, Dk Abdallah Mandai anasema kuwa mbegu mbichi za alizeti ni tiba ya mishipa ya fahamu. mapafu mafua na kifua.

Alizeti pia zina uwezo mzuri wa kuimarisha mifupa kutokana na kuwa na madini ya ‘magnesium’ na ‘copper’ ambayo husaidia kuifanya mifupa kuwa imara.

Hali kadhalika alizeti zimesheheni vitamin E, ambayo husaidia kuondoa maumivu ya viungo katika mwili pamoja na kupambana ana miale hatari ya jua yaani 'UV rays' na hivyo kumfanya mhusika kuwa na ngozi nzuri muda wote.

Matumizi ya robo kikombe cha alizeti huweza kukuweka mbali zaidi na uwezekano wa kushambuliwa na maradhi ya moyo, kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mafuta hatari mwilini ‘cholesterol’ hivyo kumuepusha mhusika na shambulio la moyo.

Je, unahangaika kutafuta sehemu sahihi ya kuondokana na magonjwa yanayokusumbua yakiwemo yale sugu? Kama jibu ni ndio basi fanya jitihada za kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam ili upate utatuzi wa magonjwa yanayokusumbua sasa kwa kutumia dawa za asili zisizo na aina yoyote ya kemikali. Unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443, barua pepe dkmandaitz@gmail.com
 


No comments:

Post a Comment