Wednesday, 15 April 2015

INASIKITISHA SANA NDANI YA MWEZI MMOJA TAIFA LIMEPOTEZA WATU 103 KUTOKANA NA AJALI ZA BARABARANI, HAPA KUNARIPOTI KAMILIKamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mohammed Mpinga


Imefahamika kwamba ajali za barabarani zimegharibu maisha ya watu 969 kati ya Januari mosi hadi Aprili 12 mwaka huu.


Hayo yameelezwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mohammed Mpinga amesema watu 2,500 wamejeruhiwa katika kipindi hicho, huku wengine wakibaki na ulemavu wa kudumu katika ajali hizo.

Kamanda Mpinga alisema kuwa, watu 866 walikufa na wengine 2,363 kujeruhiwa kati ya mwezi Januari na Machi, huku watu wengine 103 nao walipoteza maisha na 138 kujeruhiwa kati ya Machi 11 na Aprili 12 mwaka huu.

Kamanda  Mpinga alisema katika ajali hizo zote chanzo kikubwa kimekuwa ni mwendo kasi wa madereva bila kuzingatia alama na michoro ya barabarani na abiria kushabikia mwendokasi na kumtetea dereva pindi anapofanya makosa.

“Dereva akifanya makosa akikamatwa abiria wanachangia kumlipia faini dereva jambo ambalo linawapa madereva kiburi wakiamini akifanya makosa abiria wanamsaidia” alisema Kamanda Mpinga. 

Mbali na sababu hiyo, pia madereva wamekuwa na sababu za kuendesha kibabe barabarani pindi wanapokutana na magari madogo, kitendo alichosema si sahihi kisheria na kinaweza kuchangia ajali hivyo ni vyema kila mmoja kumheshimu mwenzake na kufuata sheria.

Pia alisema jambo lingine linalosababisha ajali za barabarani ni matumizi ya dawa za kulevya na ulevi mambo ambayo humfanya dereva kuchoka na matokeo yake kusababisha ajali.

Aidha, aliwataka madereva kuwa na tahadhari wanapoendesha hususani vipindi vya mvua, akiwahimiza kuwa waangalifu na kuzingatia michoro na alama za barabarani na abiria kutoa taarifa za madereva wanaokwenda kinyume na sheria za barabarani.

Ajali ya basi na lori iliyotokea mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Msimba kwenye Barabara Kuu ya Morogoro – Mbeya, kilometa chache kutoka Ruaha Mbuyuni na kusababisha abiria hao 18 kuungua vibaya.
Kufuatia matukio hayo ya ajali pia Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutengwe kuomboleza vifo vya watu 19 na wengine 11 waliojeruhiwa katika ajali ya basi na lori iliyotokea mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Msimba kwenye Barabara Kuu ya Morogoro – Mbeya, kilometa chache kutoka Ruaha Mbuyuni na kusababisha abiria hao 18 kuungua vibaya.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, alisema: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 18 kutokana na ajali mbaya ya barabarani iliyosababisha miili yao kuungua vibaya"

“Huu ni msiba mkubwa kwa Taifa, hivyo nakutumia salamu zangu za rambirambi, na kupitia kwako naomba salamu zangu za rambirambi na pole nyingi ziwafikie pia wanafamilia, ndugu na jamaa waliopotelewa na wapendwa wao katika ajali hiyo."

"Namuomba Mola awape moyo wa uvumilivu na subira watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa zao katika ajali hiyo mbaya."

"Vilevile namuomba Mola awawezeshe majeruhi wote wa ajali hiyo kupona haraka, ili warejee katika hali yao ya kawaida na kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao,” aliongeza kusema Rais Kikwete.


Mandai Herbal Clinic pia tunaungana na Watanzania wote kutoa pole za dhati kwa wale wote waliopoteza wapendwa wao katika ajali hizo na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi wote.
 

No comments:

Post a Comment