Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 14 April 2015

JE, ULIWAHI KUWAZA KUWA PILIPILI INAWEZA KUWA NA MSAADA WOWOTE MWILINI MWAKO?Kama ilivyo kwa matunda na vyakula vingine kuwa na faida kiafya mwilini, pilipili nayo ipo kwenye orodha.


Licha ya kuwa baadhi ya watu hugopa sana matumizi ya pilipili, lakini ina kiasi kikubwa cha vitamin C.

Kumekuwa na baadhi ya watu wakisema kwamba pilipili humfanya mlaji kujiamini, jambo ambalo halina uthibitisho wa kutosha, lakini pilipili pia inadaiwa kudhibiti uzito, licha ya kuwa haijathibitishwa rasmi kama inaweza kupunguza uzito wa mwili. 

Pia pilipili inaaminika kwa kuwa na uwezo wa kudhibiti maumivu ya viungo , lakini pia huwasaidia wale wenye tatizo la kukosa hamu ya kula na kuwafanya kupata hamu ya kula.

Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani na Chama cha Watafiti wa Ugonjwa wa Saratani, uligundua kuwa upo uwezekano wa pilipili kuua na kutokomeza viini vya saratani ya uzazi na mapafu, endapo italiwa chini ya usimamizi na maelekezo ya daktari.

Faida hizo za pilipili huweza kupatikana kwa kuhakikisha mlo wako unakuwa na kiwango kidogo cha pilipili utakachoweza kukimudu.Pia ni vyema ukatumia pilipili halisi na siyo ya kwenye makopo.

Unaweza kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Au wasilina na Dk Mandai kwa mawasiliano yafuatayo: 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila sikuNo comments:

Post a Comment