Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 11 April 2015

JE, UMELISIKIA AGIZO LA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) KUHUSU OPERESHENI WAKATI WA KUJIFUNGUA KWA KINAMAMA?

Ni wazi kwamba kinamama wengi wajawazito miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakijifungua kwa njia ya upasuaji zaidi kuliko ile njia ya kawaida.


Kutokana na kushamiri kwa hali hiyo Shirika la afya duniani, (WHO) limeonya kuhusu utamaduni huo ulioshamiri kwa sasa kwa baadhi ya madaktari na wanawake kupenda huduma ya upasuaji wakati wa kujifungua.

Shirika hilo limesema kuwa licha ya umuhimu wa huduma hiyo pia ni muhimu kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto, lakini ni lazima izingatie vigezo vyake.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, Dokta Marleen Temmerman wa WHO amesema ni dhahiri kuwa uzazi kwa njia ya upasuaji unaweza kuokoa maisha, lakini mara nyingi hufanyika bila ulazima, huku madaktari na wazazi wakiona njia hiyo ni rahisi kuliko kujifungua kawaida.

Dkt,Temmerman amesema kwamba, njia ya upasuaji inapaswa kutumika iwapo kujifungua kwa njia ya kawaida kunahatarisha maisha ya mama kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchungu kupitiliza au mtoto hayupo katika nafasi nzuri ya kutoka kawaida. 

"Hatupaswi kufanya upasuaji kwa kila mama anapojifungua. Jambo muhimu ni kwamba tunaamua njia ya kujifungua kawaida na tunaamua tu upasuaji iwapo kuna umuhimu kwa ajili ya afya ya mama na mtoto." alisema Dkt Temmerman.

Miongoni mwa madhara yatokanayo ya kujifungua kwa upasuaji ni kutoka damu kupita kiasi, ulemavu na hata kifo iwapo huduma hiyo itafanyika katika maeneo yasiyo na vifaa vya kutosha na salama.


Unaweza kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Au wasilina na Dk Mandai kwa mawasiliano yafuatayo: 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku


No comments:

Post a Comment