Saturday, 11 April 2015

JE, UMEWAHI KUSIKIA KUHUSU HUU UGONJWA UITWAO USONJI? YAPO HAPA MAELEZO YAKE KARIBU
Hivi uliwahi kusikia ugonjwa huu unaoitwa Usonji, au kwa kiingereza autism?


Kama hujawahi kusikia ugonjwa huu basi taarifa ni kwamba, ugonjwa wa usonji ni ugonjwa ambao huwakumba zaidi watoto wadogo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani, (WHO) wanasema kwamba ugonjwa huu humkumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani. 

Usonji ni tatizo la kibaiolojia analopata mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake na dalili huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea.

Kabla ya hapo wataalam wanasema ni mara chache sana kuona dalili hizo, ambapo zinapojitokeza mtoto hukosa mbinu za uhusiano na kushindwa kuzungumza na wakati mwingine kurukaruka na hata kujing'ata.

Watoto wenye tatizo hili baadhi yao hutelekezwa na jamii na kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa.

Hata hivyo kama ilivyo kwa baadhi ya magonjwa kutengewa siku maalum ya kutoa uelewa zaidi kuhusu ugonjwa fulani hivyo hivyo pia Usonji umepewa siku yake , ambayo ni  April 2 kila mwaka.

Ili jamii kuufahamu zaidi ugonjwa huu, Umoja wa Mataifa umetaka elimu zaidi itolewe kwa jamii  ili ibadili mtazamo kwani watoto wenye usonji wakipatiwa huduma mapema wanaweza kushiriki vyema katika jamii zao kwani wana uelewa wa hali  ya juu.

Hapa nchini Tanzania harakati za kuelimisha jamii kuhusu Usonji zilikwishaanza huko Kilimanjaro na Arusha, ambapo mtazamo unabadilika. 


Unaweza kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Au wasilina na Dk Mandai kwa mawasiliano yafuatayo: 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku


No comments:

Post a Comment