Wednesday, 1 April 2015

JE, UNAFAHAMU KUHUSU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME? TUMIA NAFASI HII KUFAHAMU HAPA

Imekuwa ni kawaida sana kwa sasa ukikatiza katika maeneo mbalimbali hapa nchini kukutana na vibao vya matangazo kuhusu kutoa dawa na tiba ya tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume licha ya kuwa Serikali imekuwa ikikemea utaratibu huo wa vibao.


Lakini kwa tafsiri ya haraka haraka kuwepo kwa vibao hivi kunamaanisha kwamba ni kweli kuna ukubwa wa tatizo hilo kwa wanaume walio wengi na ndio maana baadhi ya watu wanatumia nafasi hiyo kuweka mabango yao jambo ambalo si sahihi pia kiutaratibu.

Hivyo leo nimeona ni vyeama tuangazie tatizo hili la ukosefu wa nguvu za kiume ili kujua linachangiwa na nini hasa.

Hapo awali tatizo hili lilionekana kuwekumba zaidi watu wenye umri mkubwa (wazee) lakini kwa sasa si wazee pekee ndio hukabiliwa na tatizo hilo bali hata vijana wamejikuta wakiwa ni waathirika wa tatizo hilo.

Moja ya sababu ya tatizo hili ni magonjwa, mfano wa magonjwa hayo ni pamoja na kisukari, wanaume wanaougua maradhi ya kisukari wana hatari mara tatu zaidi kukosa nguvu za kiume kuliko wanaume wasio na maradhi hayo. Sukari isipodhibitiwa katika damu, huharibu neva na misuli midogo inayodhibiti kusimama kwa uume.

Pia watu wenye msongo wa mawazo huwa katika nafasi kubwa ya kukumbwa na shida hii ya nguvu za kiume na mara nyingi msongo wa mawazo huweza kusababishwa na unasababishwa na migogoro ya kifamilia, ufukara au imani za kishirikina.

Hali kadhalika matumizi ya madawa bila kupata maelekezo kutoka kwa wataalam huweza kuchangia tatizo hili kwa wanaume, hivyo ni vizuri kuhakikisha unatumia dawa mara baada ya maelekezo kutoka kwa wataalam husika (pharmacist).

Pamoja na hayo, vyakula unavyokula kila siku navyo ni moja ya sehemu ambayo huweza  kuchangia tatizo hili, hususani pale unapokuwa unakula vyakula visivyo na virutubisho vya kutosha tena kila siku.

Hizo ni sababu chache tu zinazoweza kupelekea tatizo hili, lakini endelea kuwa karibu na tovuti hii kila siku nitaendelea kukueleza mambo mengine juu ya suala hili, pia kama unatatizo hili unaweza kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhu la tatizo hilo. Au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment