Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Wednesday, 22 April 2015

JE, UNATATIZO LA KUSAHAU? KAMA JIBU NI NDIO BASI NI VYEMA UKASOMA HAPABaadhi ya watu wamekuwa na shida ya kusahau mambo mara kwa mara hasa wale wenye umri mkubwa na baadhi yao wa umri wa makamo.


Leo kuna baadhi ya njia hapa ambazo zikitumika vizuri huweza kusaidia kupunguza au hata kumaliza kabisa tatizo la kusahau.

Pilipili Manga, ni moja ya njia hiyo, ambapo mhusika atapaswa kuchukua kijiko cha chai cha unga wa pilipili manga kisha kuchanganya na kijiko kimoja cha chai cha asali na kisha kuanza kutumia kwa kulamba polepole kila asubuhi na jioni.

Matumizi ya maua ya komamanga nayo yapo kwenye orodha ya matunda yanayoweza kutoa auheni kwa mtu mwenye tatizo hili, ambapo utahiitaji kukusanya machipukizi ya maua ya komamanga  na kuyakausha katika kivuli kisha baadaye kuyasaga hadi yawe unga na kutunza unga huo katika chupa safi yenye  mfuniko.

Pamoja na njia hizo kuwa na uwezo wa kutoa ahueni kwa watu wenye tatizo hilo pia ni vyema njia hizo zikaenda sambamba na kuzingatia kupata muda wa kupumzika vizuri pamoja na kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha na kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 


No comments:

Post a Comment