Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 22 April 2015

JIFUNZE KUKABILIANA NA HOFU KATIKA MAISHAHofu ni moja ya mambo ambayo huwakumba baadhi ya watu, kuna watu ambao wameathiriwa na suala hili la hofu katika masuala yao mbalimbali yakiwemo masuala ya elimu, kikazi, afya na hata kiuchumi.


Kuna badhi ya watu pia wameshindwa kufikia malengo na ndoto zao katika maisha kutokana na kuwa na hofu na mashaka.

Tunapozungumzia hofu ni kwamba ni ile hali ya kujali pasipo na sababu ya msingi au kusiko na maana yoyote.

Ukizungumzia suala hili la hofu kuwa ni kutokujali pasipo kuwa na msingi ni kwa sababu zifuatazo.

Mtu kupoteza tumaini na imani aliyonayo juu ya ufanisi wa jambo fulani, hii inamaana kama hofu katika jambo fulani huishinda imani aliyonayo na hivyo hali ya kushindwa kuonekana zaidi kuliko hali ya kushinda.

Hofu pia huweza kujitokeza kwa mtu kutokana na kuweka mawazo zaidi katika vitu ambavyo viko nje ya uwezo wake.

Hofi pia huchangiwa na tabia ya kuwaza mambo yajayo badala ya kujipanga na kujiandaa kuyakabili pale yatakapofika.

Kuweka msisitizo zaidi katika jambo moja na kusahau mengine. Mara zote mtu mwenye hofu hudhani kwamba huenda ikiwa kile anachokiwekea msisitizo kitashindikana, basi kila kitu kitakuwa kimeharibika.

Yafuatayo yatakusaidia kupunguza kiwango cha hofu katika maisha yako.

Jambo la kwanza inakupas kujiuliza swali hili, Je, ni kitu gani umekipa umuhimu zaidi katika maisha yako, Je ni kazi yako?, Je ni elimu yako?, Je ni watoto wako au mwenzi wako?, Je ni malipo ya mkopo uliochukuwa?,  Lazimaukumbuke kuwa hata ukiwaza kiasi gani juu ya masuala hayo haitakusaidia wala kukuongezea chochote.

Hivyo baada ya kusema hayo kikubwa kinachohitajika katika kukabiliana na hofu ni kuacha kuyapa mawazo yako au mitazamo yako umuhimu usio stahili. Uonapo unakuwa na woga wa mara kwa mara basi jua wazi kwamba wewe unayapa mawazo, fikra na mitazamo isiyostahili.

Tabia sugu nyingi walizonazo watu husababishwa na fikra, vile unavyowaza usiruhusu mawazo yako yakufanye mtumwa.

Mawazo ya kitaaluma yanaonesha kwamba kama ukiweka mawazo yako sana katika kitu Fulani, inaweza kuishawishi tabia au utendaji wako katika hali ambayo yaweza kuanza kufanya hofu zako kuanza kuwa kweli.

Ni kwasababu hii ndiyo maana unashauriwa kuweka mawazo na fikra zako zote kwenye vitu ambavyo havina maana. 

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment