Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 29 April 2015

KIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA, HAPA NIMEKUWEKEA LIST YA MBINU ZA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA NGONOVijana ni kundi ambalo liko katika hatari zaidi ya kupata maambukizi  ya magonjwa ya ngono kutokana na kuwa na hisia kali za kupenda  na  pia  hamu  ya  kufanya  tendo  la  kujamiiana hujitokeza kwa nguvu kutokana na kukua.


Hali hiyo huchochewa na vichocheo /homoni   vilivyomo mwilini ambavyo katika kupanda na kushuka husababisha hisia za kufanya tendo la kujamiiana.

Hivyo basi vijana ni moja ya kundi ambalo endapo watakosa ufahamu wa kutosha kuhusu milli yao wanaweza  kujiingiza  katika tabia hatarishi  za kujamiana hovyo pasipo kuchukuwa tahadhali ya kupata magonjwa ya ngono.


Mandai Herbal Clinic kwa kutambua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya taifa lolote tumeona ni vyema leo tukafahamishana hizi mbinu za kupambana na magonjwa ya ngono kwa vijana:

Ili kuepukana na maambukizi ya magonjwa ya ngono zingatia yafuatayo:

  • Epuka kufanya tendo la kujamiana katika umri

mdogo

  • Epuka ulevi na matumizi ya dawa ya kulevya
  • Jiepushe na vitendo vya ubakaji

  • Jihadhari na kupiga denda ‘romance’  na mwenzi usiyejua hali
yake ya afya
  •   Jiepushe na vitendo vya kunyonya uume au uke wa
mwenza
  •  Tumia muda wako mwingi katika masomo, kazi za
mikono, michezo na sanaa
  •   Epuka makundi ya vijana walevi, wazururaji na
wavuta bangi au watumiaji wa madawa ya kulevya

  • Epuka vishawishi kama zawadi na lifti za magari

barabarani
  • Tumia kondomu ya kike au ya kiume kwa usahihi
kwa kila tendo la kujamiana

Karibu Mandai Herbal Clinic, tunatibu magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya ngono pamoja na matatizo ya U.T.I sugu. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment