Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 24 April 2015

KUELEKEA SIKU YA MALARIA DUNIANI, KUNA TAARIFA KUTOKA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI IMETOKA IKO HAPA
Kuelekea siku ya Malaria duniani tarehe 25 mwezi huu, Shirika la afya duniani, WHO wiki hii litatangaza miongozo iliyoboreshwa ya tiba dhidi ya Malaria ambayo pamoja na mambo mengine inajumuisha mapendekezo ya kinga ya ugonjwa huo dhidi ya wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.


Shirika hilo lomesema hatua hiyo ni muhimu ili kuondoa pengo kati ya tiba na kinga na kwa kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana kwenye kupunguza vifo vitokanavyo na Malaria bado watoto na wajawazito hususani barani Afrika hawapati tiba sahihi inayopendekezwa.

Hata hivyo, uchunguzi wa kina unahitajika ili tiba dhidi ya Malaria iwafikie wale wenye Malaria na hasa watoto na wajawazito na si vinginevyo, huku lengo likiwa ni kupunguza vifo vya asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 na asilimia 90 mwaka 2030.

Pamoja na hayo, suala linalotia shaka kwenye vita dhidi ya malaria ni pamoja na uwepo wa dawa bandia, ambapo watu milioni 60 hawapati dawa sahihi dhidi ya Malaria.

Naye mtaalam wa afya Peter Olumese kutoka WHO alisema kuwa “ubora wa dawa, suala la dawa bandia na zisizokidhi viwango bado ni tatizo kubwa na kwenye miongozo hii jambo muhimu ni kuhakikisha dawa ni za ubora na viwango vinavyotakiwa."

Sambamba na hayo ujumbe wa siku ya Malaria duniani mwaka huu ni wekeza katika mustakhbali, tokomeza Malaria.

No comments:

Post a Comment