Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 13 April 2015

KUNA MATUKIO MENGINE YANAPOTOKEA NI LAZIMA YATAKUSHANGAZA PALE UNAPOYASIKIA, LEO KUNA HILI TUKIO LA MWANAMKE WA MIAKA 65 KUBEBA MIMBA TENA YA PACHA WANNE!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 kutoka Berlin Ujerumani ambaye ana watoto kumi na watatu ametangaza kuwa ni mjamzito na pacha wanne.


Taarifa zinasema kuwa mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Annegret Raunigk, ambaye pia ni mwalimu wa kingereza na kirusi kwa mwaka mmoja na nusu sasa amekuwa akijaribu kupata mtoto mwingine kwa njia ya upandikizaji.

Vyombo vya habari vya German RTL vimeripoti kwamba bibo huyo alilazimika kuwatafuta watoto zaidi baada ya kitinda mimba wake mwenye umri wa miaka 9 kumsihi umtafutia watoto atakaocheza nao.

Hata hivyo, pamoja na Bi Raunigk, kuhitaji mtoto mmoja tu, lakini Mwenyezi Mungu ameamjalia mimba ya watoto wanne na wala siyo mmoja kama alivyotarajia na sasa mimba yake hiyo ina wiki 21.

Hadi sasa Bi Raunigk amejaliwa kuwa na wajukuu saba huku mimba yake hiyo ya kihistoria ikiwa haijaonesha hitilafu yoyote.

Kufikia sasa mwanamke ambaye anashikilia rekodi ya kujifungua akiwa na umri mkubwa zaidi ni Omkari Panwar, kutoka India aliyejifungua akiwa na miaka 70.

Tutembelee Mandai Herbal Clinic ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na hakika utapata suluhisho karibu sana. Wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.


No comments:

Post a Comment