Wednesday, 8 April 2015

KUNA ULE USEMI USEMAO MWANAMKE NYWELE, YAPO HAPA MAMBO MUHIMU YATAKAYO KUSAIDIA KUTUNZA NYWELE ZAKO.
Tunajua kuwa wanawake wengi hupenda masuala ya urembo nakupendeza kwa ujumla.Moja ya mambo muhimu kwa wanwake walio wengi katika masuala ya urembo ni suala la kutunza nywele zao ili ziwe katika muonekano mzuri.

Lakini kwa bahati mbaya, kuna baadhi ya wanawake hukabiliwa na tatizo la kuwa na  nywele dhaifu, na zisizo na muonekano mzuri.

Katika suala la kuwa na nywele nzuri na zenye afya moja ya mambo muhimu ni pamoja na kupata lishe nzuri. Hivyo ni vyema ukajenga utaratibu wa kula chakula chenye virutubisho sambamba na maji mengi.

Pia ni vyema ukajenga utaratibu wa kutumia mafuta yanayotokana na mimea kwa ajili ya kurutibisha nywele (mfano mafuta ya nazi asilia).

Uvaaji wa mawigi kama njia ya kuonekana mrembo si njia nzuri kwani huzifanya nywele halisi kukosa hewa na hivyo kunywea sana na kutofurahia urembo wako.

Anza sasa kwa kupenda nywele zako kwani kumbuka kwamba muonekano wa 
mwanamke kwa kiasi kikubwa ni nywele, na unapokuwa na nywele asili zenye afya hukufanya kujisikia vizuri.

Je, unahitaji kuuliza swali lolote kwetu? kama jibu ni ndio basi hakikisha unalike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic -mhc na utakuwa na uwezo wa kuuliza swali lolote kwetu ni vyema utume swali lako katika inbox kisha tutajibu swali lako pia au tuulize kupitia barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Au piga simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443

No comments:

Post a Comment