Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Monday, 20 April 2015

KUTANA NA DK MANDAI HAPA AKIKUELEZEA MAMBO MUHIMU YATAKAYOKUFANYA KUWA NA AFYA BORAAfya zetu huhitaji mambo mbalimbali ili kuwa katika hali ya ubora, hivyo kuna vitu kadhaa ambavyo huweza kuchangia afya kuwa bora zaidi.


Dk Abdallah Mandai anasema miongoni mwa mambo  muhimu katika suala hili ni pamoja na kuwa na nafasi nzuri na ya kutosha kwa ajili ya kupumzika yaani (kualala) hii ni kutokana na kuwa usingizi ni sehemu muhimu sana katika afya. Mbali ya kuwa usingizi huwa na faida kwa ajili ya afya ya akili/ubongo wetu, lakini pia ni muhimu kwa miili yetu.Afya njema huambatana na mapumziko kwani husaidia mwilii kujijenga zaidi.
 
Dk Mandai anaendelea kusema kwamba unywa wa maji kwa wingi ni muhimu sana kwa afya zetu. Ifahamike kwamba asilimia 60% ya miili yetu imetengenezwa au imesheheni maji. Hivyo maji yanahitajika kwa ajili ya kuondoa takataka au vitu visivyofaa kutoka mwilini. Hali kadhalika maji ndio hubeba virutubisho na oxygen.

Aidha, Dk Mandai anaongeza kuwa kufanya mazoezi pia ni muhimu kwa afya, jitahidi kufanya mazoezi angalau mara tatu katika wiki, ni vyema pia ukatenga muda wa kutembea japo kwa dakika 30. Muhimu zaidi ni kuchagua aina ya mazoezi unayoendana nayo. Kimsingi mazoezi ni muhimu kwa kila mtu.

Zingatia matumizi ya matunda kwa wingi, hii ni kwa sababu matunda ni chanzo kizuri cha madini na vitamin ambazo miili yetu huhitaji sana kwa ajili ya afya bora. Mfano kama machungwa yamesheheni faida kubwa zaidi kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C. Aina nyingine za matunda muhimu kwa afya ni pamoja na Parachichi (Avocado), matikiti maji, zabibu, mapapai nk.

Pia kula mboga za majani, (vegetables) ni muhimu sana kwa afya zetu. Jitahidi kupata angalau zaidi ya aina 5 za mboga za majani.

Hali kadhalika punguza kula vyakula vya viwandani, Jitahidi kuviepuka vyakula hivyo kwa kadri unavyoweza. Mara nyingi vyakula vya makopo huwa na ‘ingredients’ ambazo hazifai kwa afya zetu. Kwa mfano, miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi nyingi kitu ambacho ni chanzo maradhi ya moyo. 

Unaposhindwa kabisa kujizuia kununua vyakula hivyo vya viwandani/makopo basi jaribu kuangalia ambavyo havina sukari au chumvi.

Mbali na hayo, Dk Mandai anamalizia kwa kusema kuwa ni muhimu kujenga tabia ya kuchunguza afya zetu mara kwa mara hata pale ambapo hatujihisi kuumwa, hii husaidia kugundua hali za afya zetu mapema endapo kuna tatizo lolote na kuwa rahisi kukabiliana nalo.

Kama unasumbuliwa na magonjwa sugu pia unaweza fika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaa. Au wasiliana na Dk Mandai kwa namba za simu zifuatazo  0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443

No comments:

Post a Comment