Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Thursday, 2 April 2015

KWA WEWE UNAYEDHANI KUTEMBEA NI KUJITESA NI VYEMA UKASOMA HAPA UJUE FAIDA ZA MAZOEZI YA KUTEMBEA

Ni mara nyingi kupitia tovuti hii ya Mandai Herbal Clinic tumekuwa tukihamasishana juu ya umuhimu wa kupenda mazoezia na kufanya mazoezi.


Na tumekuwa tukifanya hivyo kutokana na kutambua umuhimu wa mazoezi katika afya zetu, huku tukishauri kuacha kupenda kutumia magari au usafiri wa aina yoyote hata katika eneo la umbali mfupi.

Hata hivyo ni wazi kwamba kuna aina mbalimbali za mazoezi ya kufanya, lakini miongoni mwa mazoezi rahisi na yasiyo na masharti makubwa ni yale ya kutembea. 

Kutembea ni njia rahisi ya kufanya mazoezi kwani zoezi hili mhusika hahitaji  vipimo vya afya ili kuweza kufanya zoezi hili, badala yake utahitaji mavazi yasiyokwaza, pamoja na mahali pa kutembelea tu.

Mara nyingi wataalamu wa afya wamekuwa wakishauri kabla ya kuanza kufanya mazoezi magumu ni vyema kupata ushauri wa daktari, lakini katika mazoezi haya ya kutembea yanashauriwa kwa mtu yeyote na mahali popote.

Wataalam wa afya, wanabainisha kuwa kutembea ni moja ya njia salama na nzuri ambayo humsaidia mhusika kuujenga na kuuimarisha moyo uwe na afya nzuri na usiwe katika hatari ya kushambuliwa na maradhi.

Wataalam wa masuala ya afya na magonjwa ya moyo wanasema kutembea ni miongoni mwa kinga ya mwili kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ukiwemo wa moyo na kiharusi.

Kutembea vilevile kunaiweka mifupa kuwa imara na kuikinga na mashambulizi ya kuzuia ugonjwa wa mifupa pamoja na kusaidia kupunguza uzito unaoongezeka bila mpangilio.


Zoezi hili la kutembea pia husaidia kuboresha usingizi na kuchochea utendaji kazi wa ubongo.

Wataalam wa masuala ya afya wanasema watu wanaotembea mara kwa mara huwa na uwezekano wa mkubwa wa kuishi muda mrefu kuliko wale wanaotumia magari kwa muda mrefu.

Pamoja na hayo mtu mwenye tabia ya kufanya mazoezi ya kutembea, hujiweka katika nafasi kubwa ya kuwa na afya nimara na njema na kutoshambuliwa na magonjwa mara kwa mara.

Anza sasa kupenda kufanya mazoezi ya kutembea angalau kwa dakika 20 kwa siku itakufanya kuwa na afya bora na imara zaidi.
Kama unasumbuliwa na magonjwa sugu pia unaweza fika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaa. Au wasiliana na Dk Mandai kwa namba za simu zifuatazo  0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443

No comments:

Post a Comment