Thursday, 16 April 2015

LEO KUNA DALILI ZA SARATANI YA NGOZI YA NGOZI HAPA (2)
Leo tunaendelea kuzungumzia ugonjwa wa saratani ya ngozi baada ya kufahamu watu walio katika hatari ya kupata saratani hii, lakini leo tutaangazia dalili za saratani hiyo. Karibu!


Moja ya dalili za saratani hii ya ngozi non- melanoma ni mgonjwa kuwa na kidonda ambacho hakiponi kwa muda mrefu  (donda ndugu)  na wakati mwingine kidonda hicho huweza kutokuwa na maumivu yoyote pia.

Hata hivyo, mara nyingi vidonda hivyo hujitokeza sehemu za mwili ambazo hazifunikwi hususani kichwani, shingoni na mabegani hii ni kutokana na sehemu hizo hupatwa na mionzi ya jua mara nyingi.

Pia kidonda cha mtu mwenye saratani kisipogundulika mapema na kupata matibabu huweza kuwa kikubwa na kusambaa hadi kufikia kwenye damu ambapo hatua hiyo inaelezwa kuwa ni hatari zaidi kwani huweza kusababisha kifo.

Hayo ndio macheche kuhusiana na dalili za saratani hii ya ngozi, lakini nikusihi endelea kutembelea tovuti hii (www.dkmandai.com ) kila siku kwani nitaendelea kukuletea maelezo kuhusu ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na namna ya matibabu yake.

Karibu Mandai Herbal Clinic kama unasumbuliwa na magonjwa sugu au unahitaji ushauri juu ya masuala mbalimbali ya kiafya. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku

No comments:

Post a Comment