Tuesday, 21 April 2015

LEO KUNA HIZI FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA NIMEKULETEA HAPA
Maboga ni moja ya chakula bora na muhimu kwa siha ya mwili wa mwanadamu, leo Mandai Herbal Clinic tunakusegezea hizi faida 5 za kula mbegu za mabogaKwanza kabisa mbegu za maboga huweza kusimama kama kinga ya mwili, hii ni kutokana na kuwa na kiwango kizuri za madini aina ya zink, ambayo yanafaida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa kinga ya mwilini, kuweka macho na ngozi vizuri pamoja na kuimarisha ukuaji wa seli, Hali kadhalika zinki huimarisha nguvu za kiume.


Mbegu za maboga huwa kiwango kingi cha madini aina ya magnesium, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja na mishipa ya damu, huku ikiongeza ufanisi wa utumbo mpana


Aidha, kwenye mbegu za maboga pia huwa na kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo mbegu hizi zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.


 Kama hapo awali tulivyosema kuwa mbegu za maboga huwa na madini ya zinki mengi, hivyo baadhi ya tafiti zimekuwa zikiainisha kwamba mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.


Kwa wale wenye matatizo ya kuvimba miguu au sehemu mbalimbali za mwili, hii ni kutokana na mbegu hizo za maboga kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, ikiwa ni pamoja na majipu.

Ili kutumia mbegu hizi kama tiba unapaswa kuhakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizo safi ambazo hazijakaa muda mrefu, lakini pia tumia mbegu hizo kwa usalama zaidi ikiwa ni sambamba na kuziosha na maji safi na salama kisha zianike na inapendeza zaidi ukila bila kukaanga


Asante kwa kuendelea kuwa karibu nasi, tafadhali endelea kulike page yetu ya facebook zaidi iitwayo Mandai Herbalist Clinic –mhc ili taarifa zote za tiba asilia na mimea ziwe zinakufikia mapema. Pia kama una tatizo lolote la kiafya wasiliana
0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 


No comments:

Post a Comment