Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 29 April 2015

LEO NI DALILI ZA UGONJWA WA FIGO (2)Jana tulianza kuzungumzia kuhusu tatizo la figo ambapo tuliangazia baadhi ya sababu ambazo huchangia kuharibika kwa figo. Sasa leo tutaangalia daliliza ugonjwa wa figo.


Kwa kawaida mwanzoni, ugonjwa wa figo huwa hauoneshi dalili yeyote, lakini mara utendaji kazi wa figo unapopungua, dalili hujitokeza kuendana na udhaifu.

Aidha, dalili nyingine za mwanzo ni pamoja na kuchoka mara kwa mara, mwili kukosa nguvu, kukosa pumzi na kupumua kwa shida, kudhoofika na kuvimba mwili (hasa usoni) pamoja na homa isiyokuwa kali

Ushauri wa lishe na ulaji kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo
Ulaji wa mtu mwenye ugonjwa wa figo unapaswa kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwani figo haziwezi tena kutoa mabaki ya protin, maji, chumvi na potassium kwa urahisi inapozidi mwilini. Vyakula vyenye chumvi na potassium nyingi viepukwe.


Mbali na hayo mgonjwa anahitajika kuzingatia kupunguza kiasi cha nishati lishe, pale inapotokea kiasi cha nishati lishe na protini kikazidi mwilini huzipatia figo ambazo zimeathirika kazi kubwa.

Hata hivyo, wagonjwa wa figo huhitaji vitamin na madini ya nyongeza kutokana na kutokula aina mbalimbali za vyakula na hivyo kuweza kusababisha upungufu wa baadhi ya virutubishi. Damu inapochujwa (dialysis) pia huondoa vitamin kwenye damu. Virutubishi vya nyongeza vitolewe kwa mgonjwa wa figo kwa ushauri wa daktari.
 

Mandai Herbal Clinic inapenda kukujuza kwamba kama unateseka na magonjwa mbalimbali kwa muda mrefu sasa ni mwisho, unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unafika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na upate matibabu sahihi kwa kutumia tiba asilia za mimea na matunda. Wasiliana nasi sasa kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 


No comments:

Post a Comment