Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 2 April 2015

LEO NIMEKULETEA HII YA MBEGU ZA TIKITI MAJI KUTUMIKA KAMA TIBA
Tikiti maji ni moja ya tunda ambalo linapendwa sana, lakini pia ni moja kati ya matunda yenye maji mengi na matamu  ndani yake.


Mbali na kuwa na maji yenye ladha nzuri  pia tunda hili linafaida kadhaa katika masuala ya afya hususani pale linapotumika ipasavyo.

Leo tutaangalia faida za mbegu za tunda hili ambapo Mtaalam wa tiba asili hapa nchini Dk Abdallah Mandai, anasema ni miongoni mwa mbegu zenye kiwango kikubwa cha protini.

Aidha, anasema kuwa mbegu hizo zina vitamin B ambayo ni muhimu pia mwilini kwani husaidia kubadili chakula kuwa katika mfumo wa nishati.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anasema kwamba mbegu hizo zinauwezo mzuri wa kusaidia katika mmeng’enyo wa chakula pamoja na mfumo wa fahamu, huku zikisaidia pia kuimarisha afya ya ngozi kwa mtumiaji.
Tunda la tikiti maji likiwa na mbegu zake
 Pia mbegu hizi za tikiti zinasifa ya kuwa na kiwango kizuri cha madini ya ‘magnesium’ ambayo husaidia kuthibiti shinikizo la damu, hali kadhalika ndani yake kuna madini ya chuma, ‘zinc’, 'sodium' na 'manganes.’

“Mbegu zake zinapoliwa husaidia kushusha shinikizo la damu na zikikaangwa na kusagwa huwa ni dawa ya maumivu wakati wa kujisaidia,” alisema Dk Mandai

Sambamba na hayo, Dk Mandai anaongeza kwamba mbegu za tikiti maji zikikaangwa na kisha kusagwa na mgonjwa akanywa huweza kutibu kifua kikuu  kwa mhusika endapo mhusika  atakuwa akitumia vijiko viwili kutwa mara mbili.

Kama unasumbuliwa na magonjwa sugu pia unaweza fika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaa. Au wasiliana na Dk Mandai kwa namba za simu zifuatazo  0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443

No comments:

Post a Comment