Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 26 April 2015

MAAJABU YA MAJANI YA MUEMBE KATIKA TIBAKisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya mfumo wa uyeyushwaji wa chakula ndani ya mwili.Ukosefu au upungufu wa kemikali inayoitwa insulin husababisha ongezeko la sukari inayojionesha kwa kiwango kikubwa katika haja ndogo ya muathirika pia.

Miongoni mwa sababu ambazo hupelekea ugonjwa huu ni pamoja na kuishi maisha ya anasa, watu wasiojishughulisha na kazi za kutumia nguvu au mazoezi na wale wanaopenda kutumia vyakula vilivyotengenezwa kwa kuongezwa sukari.

Dalili za mtu mwenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja na kukojoa mara kwa mara, kuhisi njaa mara kwa mara, kuhisi kiu ya maji mara kwa mara, kupungua uzito wa mwili pamoja na kuchoka kwa mwili  mara kwa mara.

Matibabu ya ugonjwa wa kisukari hayalengi katika kuponya ugonjwa , ila ni kumsaidia mgonjwa aweze kuishi maisha ya kawaida.

Moja ya tiba asili inayoweza kumsaidia mgonjwa wa kisukari kuishi maisha ya kawaida ni hii ya matumizi ya majani ya mwembe.

Dk Mandai anabainisha kuwa majani haya yanapokuwa machanga na kulowekwa  ndani ya maji safi na salama  kisha kukamua maji hayo na kunywa glasi ya maji hayo humsaidia sana mgonjwa wa kisukari.

Njia nyingine ni kukausha majani ya mwembe kupitia kivuli kisha baada ya kukauka vizuri saga yawe unga laini na utumie kijiko cha chai katika glasi ya maji mara tatu kwa siku.

Pia zambarau huweza kumsaidia mgonjwa wa kisukari hii ni mara baada ya kuzikausha na kuzisaga ili kupata unga laini, kisha tumia nusu kijiko cha chai cha unga wa zambarau katika glasi ya maji kila siku asubuhi kabla ya kula chochote.

Pamoja na tiba zote zilizoorodheshwa hapo juu mazoezi ya viungo ni muhimu kila siku, mazoezi hayo ni pamoja na kutembea na kukimbia na mazoezi ya viungo pia ni vyema ukazingatia kutumia mboga za majani.

Lakini ni vyema ukafika kliniki kwetu Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment