Wednesday, 8 April 2015

MATATIZO YA KUOZA MENO KWA WATOTO NA NJIA YA KUKABILIANA NAYOTatizo la kuoza kwa meno ni moja ya tatizo ambalo huwakumba watoto wengi katika kipindi cha ukuaji wao.


Mbaya zaidi tatizo hili husababisha watoto wengi meno kushambuliwa kwa mpigo hasa kuanzia meno ya juu na mbele.

Katika tatizo hili mara nyingi meno ya chini na mbele ni mara chache kushambuliwa kwa kutokana na kukingwa na visababisha vya kuoza na ulimi.

Kuna baadhi ya sababu zinazochangia kuoza kwa meno kwa kasi katika kipindi cha utoto sababu hizo ni pamoja na tabia ya ulaji ya mtoto (feeding habits). Watoto wengi hupenda kunywa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na mara nyingi.

Watoto walio kwenye hatari zaidi ya kuoza kwa meno ni wale wa watoto wa wazazi wenye shughuli nyingi na hivyo kulazimika watoto kutumia chupa za kufyonzea kwa muda mrefu ambao hawapo nao. Pia watoto wenye kutumia dawa zenye sukari mara kwa mara.
 
Hali kadhalika watoto wale ambao huachishwa kunyonya mapema zaidi huwa katika hatari ya kuoza kwa meno kutokana na kutumia chupa kama mbadaala wa zoezi hilo.

Unaweza kumuepusha mtoto kuoza meno kwa kupunguza matumizi ya chupa za kufyonzea

Mzazi unapaswa kujenga utaratibu wa kumkagua mtoto wako kinywa mara kwa mara na unapoona tatizo ni vyema ukampeleke hospitali mapema.

Pia mzazi unashauriwa kudhibiti matumizi ya vinywaji na vitu vya sukari mara kwa mara.

Acha kuumizia kichwa kuhusu sehemu ya kwenda pale unaposumbuliwa na magonjwa mbalimbali, kumbuka kuwa Mandai Herbal Clinic ipo kwaajili yako. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam, au tupigie simu namba  0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment