Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 23 April 2015

MATATIZO YA VIDONDA VYA MDOMONI NA NAMNA YA KUKABILIANA NAYO
Je ni mara ngapi umewahi kujikuta ukikubwa na tatizo la kutokwa na vidonda mdomoni?


Basi ni vyema ikafahamika kuwa tatizo hili limekuwa likiwakuta baadhi ya watu katika jamii zetu tunazoishi na hivyo kumsababisha mhusika kupata maumivu makali na hata kusababisha kushindwa kuongea vizuri.

Vidonda hivi huweza kusababishwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuna kwa muda mrefu (bigijii), uvutaji wa sigara, maambukizi ya virusi, bacteria na fangasi, lakini pia na ukosefu wa virutubisho vya zink, vitamin C, vitamin B 12 na madini ya chuma.

Unaweza kuepuka na tatizo hilo kwa njia zifuatazo:
Pendelea kunywa juisi ya matunda mbalimbali itakayo kupatia virutubisho mbalimbali na madini ambayo huongeza kinga mwilini.

Epuka kula vyakula na vinywaji vya moto au baridi sana kwani huweza kuchangia kuchelewa kupona kwa vidonda.

Kunywa maji mengi kila siku ambayo si ya moto wala ya baridi.
Hakikisha unapiga mswaki mara kwa mara na taratibu ili kuepuka kukwangua sehemu zenye vidonda.

Tumia asali ambayo husaidia kuua vimelea na kuponya makovu huku ikilainisha sehemu zenye vidonda.

Tumia maji ya nazi (madafu) ambayo hupooza mwili na kuua wadudu hatari mdomoni, hali kadhalika unweza kupaka mafuta ya nazi kwenye sehemu yenye kidonda ili kupona haraka.

Zingatia kwamba vidonda visivyopona kwa muda zaidi ya wiki mbili huku ukiwa umejaribu tiba hizo hapo juu basi hio ni ishara ya tatizo kubwa, hivyo inakupasa kwenda hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam zaidi. 

 Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment