Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 29 April 2015

MATUMIZI YA NYANYA NAYO YAKIPEWA KIPAUMBELE YANAFAIDA KATIKA AFYA ZETUHabari za leo mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa tovuti hii ya www.dkmandai.com karibu tuendelee kufahamishana mambo mbalimbali kuhusu afya zetu.


Leo nimeona tufahamishane haya machache kuhusu nyanya na faida zake katika afya.

Wengi wetu tunaifahamu nyanya kama kiungo kwenye mapishi yetu au hata kachumbari kwenye mlo.

Hata hivyo, watafiti nchini Marekani wamebaini kuwa wanawake wanaokunywa juisi ya nyanya angalau mara moja kwa wiki, wanapunguza kiwango cha kupata maradhi ya saratani ya matiti.

Kwa mfano, wanaeleza kuwa glasi moja ya nyanya kwa siku ina kiwango sahihi na cha kutosha cha madini ya 'Lycopene,' ambazo ni kemikali za mimea zinazoaminika kuondoa kukua kwa saratani.

Kimsingi madini ya Lycopene ndiyo yanayozipa nyanya rangi yake nyekundu na nyanya hizo zimeundwa zaidi ya vichocheo vyenye uwezo wa kuzuia saratani hiyo.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Rutgers nchini Marekani walipima, kiwango cha vichocheo kwa wanawake 70 wenye miaka 55 na kuendelea ambao walitumia juisi ya nyanya kwa wiki kumi. Wanawake hao ambao wengi walikuwa wanene kupita kiasi na baadhi wenye dalili ya saratani, walipungua uzito na saratani ilikwisha.

Kutokana na kuwa nyanya ni tunda linalopatikana wakati wowote, tena jikoni kwako, ni vyema wanawake wakajenga mazoea ya kuzitumia kama mlo hata pasipo kutengeneza juisi.


Karibu Mandai Herbal Clinic, tunatibu magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya uvimbe kwa kinamama bila kufanya upasuaji, pamoja na matatizo ya uzazi. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Acha sasa kuteseka Dk Abdallah Mandai yupo kwa ajili yako.


No comments:

Post a Comment