Mtopetope huu ni mti ambao unaweza
kuukuta umeota katika maeneo ya mabondeni au hata milimani, lakini mti huu
umekuwa ni muhimu katika kuwapatia matunda watu na inaelezwa kuwa mti huu
unamaajabu makubwa katika kutibu maradhi mbalimbali.
Kwa mujibu wa mtaalam wa tiba asili,
kutoka Mandai Herbalist Clinic , Dk Mandai anasema mti huo una maajabu makubwa
katika tiba ambapo inaonesha kuwa mti huo ulitumiwa na wazee katika kutibu
magonjwa mbalimbali kipindi cha miaka mingi iliyopita.
Magonjwa ambayo yanaweza kutibika
kupitia mti huo ni pamoja magonjwa ya wanawake hasa ya sehemu za siri.
Wanawake wenye tatizo la kutoa maji
yenye muwasho na mengine kama maziwa sehemu za siri wote wenye matatizo hayo
huweza kutibiwa kwa mti huu.
Dk Mandai anasema wanawake wanaotoa
maji yenye mwasho na mengine kama maziwa sehemu za siri wanaweza kutibiwa na
mti huu na kupona kabisa.
Dokta anaendelea kufafanunua kwamba
mara nyingi wanawake kutokana na maumbile yao wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto ya magonjwa hayo ambapo miongoni mwa athari kubwa ni kupata maumivu
makali wakati wa tendo la ndoa.
“Mwanamke ambaye ameharibika sehemu zake za
siri kutokana na uzazi mti huu ni tiba nzuri sana ambapo unatakiwa kuchemsha
majanai na kisha aoshe sehemu husika,” alisema
Dk Mandai.
Mbali na hayo, mti huo pia unasaidia
kutibu maradhi ya vidonda vya tumbo na magonjwa ya moyo ambayo yanawakabili
watu wengi hasa katika kizazi cha sasa.
Sambamba na hayo Dk Mandai anasema
magome ya mtopetope husaidia kutibu vidonda.
Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu
namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682
368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya
facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila
siku
No comments:
Post a Comment