Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 17 April 2015

MWANAMKE AWEKA REKODI YA KUJIFUNGUWA MAPACHA 5
Ni nadra sana matukio ya kujifungua watoto zaidi ya wawili au watatu na hata wanne kutokea na yanapotokea basi  huleta mshangao kwa watu wa jamii husika au nchi.


Sasa leo kuna hii taarifa ya kuzaliwa kwa mapacha watano na wote wakike huko nchini Marekani katika hospitali moja ya wanawake mjini Texas Houston.

Wauguzi katika hospitali hiyo wanasema kuwa uzazi huo kutokana na mimba moja ni rekodi mpya ambayo haijawahi kutokea Marekani.

Danielle Busby ambaye ndiye mama wa watoto hao ambao wamepewa majina ya Olivia Marie, Ava Lane, Hazel Grace, Parker Kate na Riley Paige anasema kupata watoto hao wote wakiwa wazima kwake ni baraka ya hali ya juu.

Inasemekana watoto wengi sawa na hao waliwahi kuzaliwa mara moja huko London Uingereza, mnamo mwaka 1969 katika hospitali ya Queen Charlotte.

Zaidi ya Madaktari na wauguzi 12 walilazimika kufanya kazi ya ziada ilikumsaidia bi Busby kujifungua watoto hao ambao hawakuwa wametimiza umri wa miezi tisa tumboni kwa njia ya upasuaji.

Bwana na Bi Busby wakifurahia kuwaona watoto wao

Baba wa mtoto huyo, Adam Busby ametoa sifa nyingi kwa wahudumu wote wa hospitali hiyo waliofanikisha operesheni hiyo.

Hata hivyo, taarifa zinasema kwamba Bi Busby alikuwa na tatizo la kupata ujauzito hivyo akatumia mbegu pandikizi ya uzazi

No comments:

Post a Comment