Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 14 April 2015

NAAMINI NI MUDA MREFU KIDOGO UMEPITA BILA KUSIKIA NINI KINAENDELEA KUHUSU UGONJWA WA EBOLA, KUNA TAARIFA HAPAImekuwa kama ni nadra sana kwa sasa kusikia taarifa kuhusu ugonjwa wa za ebola.


Lakini taarifa ni kwamba huko nchini Sierra Leone shule zilikuwa bado hazijafunguliwa hadi siku ya jana Aprili 13.

Shule hizo ambazo zilifungwa nchini Sierra Leone tangu mwezi Julai mwaka uliopita kutokana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola hatimaye zimefunguliwa leo hii Jumanne.

Wakati nchi humo wakifungua shule leo, mataifa mengine yalioathirika na mlipuko huo wa Ebola Magharibi mwa Afrika Guniea na Liberia wao waliruhusu kufunguliwa kwa shule zao mwanzoni mwa mwaka huu.

Baadhi ya makabuli ya watu waliofariki kwa ugonjwa wa ebola

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa Ebola bado imebaki kuwa janga la kimataifa.Pia shirika hilo limesema kwamba ugonjwa huo uliwaua karibu watu 10,600 katika mataifa hayo ya Magharibi mwa Afrika.

Takwimu za hivi majuzi zinaonesha kuwa ni visa vipya 30 vya ugonjwa wa Ebola vilivyothibitishwa nchini Guinea na Sierra Leone ikilinganishwa na mamia ya visa hivyo siku za nyuma.

Aidha, WHO inasema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuweka tahadhari kuu dhidi ya mlipuko huu ama mwengine wa Ebola.

Kuwa karibu nasi kwa kulike page yetu ya facebook iitwayoMandai Herbalist Clinic-mhc na utakuwa ukifikiwa na taarifa zetu zote kutoka kwetu.
 

No comments:

Post a Comment