Tuesday, 7 April 2015
NI AJABU NA KWELI MTOTO AZALIWA BILA PUA
Mama wa mtoto huyo aitwaye Brandi Mc Glathery aliiambia ABC News Today nchini Marekani kwamba “siku niliyojifungua, kila kitu kilikuwa sawa.''
Mama huyo aliendelea kusema kwamba, ''alipozaliwa daktari alimweka kifuani mwangu. Nilipomwangalia kwa karibu, nilisema ' Hana pua'. Walimchukua na kutoka naye.”
McGlathery alibainisha kuwa, daktari alikaa kando ya kitanda chake ili kumweleza hali ya mtoto wake. ''Alikuwa amehuzunika..''Amesema.'' Nilijua papo hapo kuwa hakuwa sawa.''
Ingawa mtoto wake hakuonesha kasoro zozote zaidi, McGlathery amesema kuwa alishangazwa na kuhuzunika kutokana na habari hizo. Lakini licha ya kukosa pua, Brown amesema kuwa mtoto huyu ana afya nzuri na pia ni mtoto mrembo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment