Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 25 April 2015

UKOSEFU WA VITAMINI WASABABISHA KUKU KUTEMBEA AKIWA KAINAMISHA KICHWA MUDA WOTE, NIMEKUWEKEA HAPA MAELEZO NA VIDEO YAKEKwa kawaida kuku ni ndege ambaye mara zote hutembea akiwa ameinua kichwa chake juu, lakini huko nchini Kenya kuna story ya kuku ambaye muda wote hutembea akiwa ameinamisha kichwa chini mithili ya mtu mwenye majonzi.

Kuku huyo ameonekana kuwa gumzo katika mji wa Kisumu nchini Kenya, ambapo hadi sasa anamiezi miwili tangua aanze kutembea akiwa ameinamisha kichwa chake.

Hata hivyo, mmiliki wa kuku hiyo anadai kwamba alishawaona wataalam wa mifugo na wakampatia dawa, lakini bado hali ikaendelea vilevile.

“Wakatupatia vitamin tuipatie tumekuwa tukiipatia sasa inaelekea two month bado inafanya hivyo, lwo nimewaita (wataalam) wamekuja wakaiona wenyewe wakatuambia kuku haina madhara yoyote kama tunaweza tuile tu”, alisema mfugaji wa kuku hiyo.

Pamoja na hayo, mfugaji huyo anasema kwamba tofauti na ilivyo kwa kuku wengine kuku huyo anaruka kama anacheza sarakasi , ambapo tukio hilo limekuwa likimpa wasiwasi mfugaji huyo hata pale wanapowaza kumchinja kwa kuhofia na wao shingo zao kupinda kama ya kuku huyo.

Taarifa hii imeripotiwa na kituo cha K24 video ipo hapa chini bonyeza play kuitazama.

  Mandai Herbal Clinic inapenda kukujuza kwamba kama unateseka na magonjwa mbalimbali kwa muda mrefu sasa ni mwisho, unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unafika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na upate matibabu sahihi kwa kutumia tiba asilia za mimea na matunda. Wasiliana nasi sasa kwa mawasiliano yafuatayo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment