Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 29 April 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA MELI MBILI KUBWA ZA KISASA ZA KIVITA, NIMEKUWEKEA PICHA ZA UZINDUZI WA MELI HIZO


 


Rais Jakaya Kikwete amezindua meli mbili kubwa za kisasa za kivita na kuzikabidhi kwa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji.

Uzinduzi wa meli hizo zenye mizinga mikubwa miwili na ya kawaida sita kila moja, na uwezo wa kupiga makombora umbali wa kilometa saba angani na kilometa tisa chini, ulifanywa jana, makao makuu ya kamandi hiyo yaliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete, alisema meli hizo zina ukubwa wa takribani meta 60 hivyo kuwezesha usalama wa uhakika katika ukanda wa bahari wa Tanzania dhidi ya maharamia.

Alisema uzinduzi wa meli hizo unaifanya Tanzania kuandika historia mpya ya kuwa na  meli za kivita na  zenye ukubwa wa jinsi hiyo kwa mara ya kwanza tangu kupatikana kwa uhuru, hivyo kurahisisha usalama wa ukanda wa bahari wa Tanzania ambao kwa sehemu kubwa ulikuwa unahujumiwa na maharamia wakiwamo wa kutoka nchini Somalia.

Meli hizo zilizopewa majina ya melivita P77 Mwitongo kuwakilisha eneo alilozaliwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere na  melivita P78 Msoga, eneo alilozaliwa Rais Kikwete.

Alisema kamandi hiyo ambayo ipo chini ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliamua kuzipa majina hayo meli hizo kwa ajili ya kuenzi utawala wa viongozi hao.

Alisema awali kamandi hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya kuwa na meli za kivita zenye uwezo wa kwenda masafa marefu kwa ajili ya kulinda rasilimali za nchi ndani ya ukanda wa bahari ya Tanzania kutokana na meli zilizokuwapo kukosa uwezo huo kwani zote zilikuwa chini ya urefu wa mita 60 ambao ndiyo unaotakiwa.

“Meli hizi zinafanya tuandike historia mpya ya kuwa na meli kubwa na za kisasa kwa mara ya kwanza nchini…..rasilimali zetu nyingi zikiwamo samaki zimeibwa sana ndani ya ukanda wa bahari yetu kutokana na meli zetu kukosa uwezo wa kukabiliana na vitendo vya uharamia dhidi ya maharamia na wezi wa samaki wetu……lakini kwa hizi, zinatuhakikishia usalama kwa arasilimali zetu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza.

Meli hizo ambazo zimepatikana kwa ushirikiano kati ya Serikali ya China.

Zina uwezo wa kusafiri siku saba umbali mrefu bila kuongeza mafuta.

Pia zina uwezo wa kupiga makombora kwa umbali wa kilometa  saba kwenda juu na chini kilometa tisa.

Kutokana na hilo, alipongeza ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, alisema, meli hizo zitakuwa tegemeo kubwa katika kulinda eneo la maji ya Tanzania na rasilimali zake ikiwamo gesi asilia  kwani zina uwezo wa kasi kubwa katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu vya uharamia.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usama nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema, lengo la kuwa na meli za jinsi hiyo ni katika jitihada za kuhakikisha jeshi la nchi linakuwa na silaha za kisasa za kivita na kutoa mafunzo.

Balozi wa China nchini, Lui Youging, alimpongeza Rais Kikwete kwa uzinduzi wa meli vita hizo kwa ajili ya kusaidia ulinzi na usalama wa nchi.Chanzo: Nipashe.

No comments:

Post a Comment