Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 28 April 2015

SABABU ZINAZOWEZA KUCHANGIA FIGO YAKO KUSHINDWA KUFANYA KAZIFigo ni moja ya kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu na hufanya kazi za kudhibiti na kuhifadhi virutubishi na maji na kuondoa mabaki kupitia mkojo.


Pia figo husaidia sana kuchuja damu ili kuondoa mabaki ambayo ni sumu mwilini. Baadhi ya mabaki hayo ni urea, uric acid, creatinine na ammonia.

Sababu zinazoweza kufanya figo zishindwe kufanya kazi:

i) Sababu za muda mfupi:
Matumizi ya baadhi ya dawa
Upungufu mkubwa wa ujazo wa damu (kupoteza damu kwa kiasi kikubwa)
Upungufu wa maji mwilini kutokana na kutapika, kuhara, na homa
Maambukizi kwenye figo mfano sepsis
Uvimbe mkubwa wa tezi dume (prostatic hypertrophy)

ii)Sababu za muda mrefu
Kisukari kisichodhibitiwa
Shinikizo kubwa la damu lisilodhibitiwa
Uvimbe-uchungu wa kudumu kwenye mfumo wa uchujaji wa figo(chronic glomerulonephritis)
Mawe kwenye figo
Magonjwa ya tezi dume (Prostate disease)

Endelea kutembelea tovuti hii nitakufahamisha dalili za ugonjwa wa figo pamoja na kukujuza lishe anayopaswa kutumia mgonjwa wa figo


KARIBU MANDAI HERBALIST CLINIC, UPATE TIBA SAHIHI NA MAKINI KWA KUTUMIA DAWA ASILI ZITOKANAZO NA MIMEA NA MATUNDA NA HAZINA KEMIKALI NA NI SALAMA KWA MATUMIZI YA BINADAMU. UNAWEZA KUWASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443 AU dkmandaitz@gmail.com. TUPO UKONGA, MONGOLANDEGE JIJINI DAR ES SALAAM.


No comments:

Post a Comment