Wednesday, 15 April 2015

SARATANI YA NGOZI SABABU ZAKE NA WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUUPATA UGONJWA HUU (1)


Saratani ya  ngozi ni ugonjwa unaotokana na matokeo ya mgawanyiko wa seli za kwenye ngozi usio na mpangilio maalum na hivyo kupelekea kuunda uvimbe unaovamia na kuathiri viungo vingine.


Mara nyingi saratani nyingi za ngozi huathiri seli kubwa mbili ambazo ni squamous cells na basal cell hivyo seli hizo zinapoathiriwahupelekea kupatwa na aina ya saratani iitwayo ‘Non Melanoma Skin Cancer’

Kimsingi kuna aina nyingi sana za saratani kwa kuzingatia ni sehemu gani ya kiungo cha mwili imeathirika, lakini aina zote hizo huwa na sifa tatu zinazofanana ambazo ni ukuaji usiothibitika wa seli.

Aidha, aina ya saratani ya ngozi inaelezwa kusababishwa na mionzi ya jua iitwayo ‘ultraviolet rays’ ambayo kitaalam huitwa (UV-B) ambayo husababisha kuharibika kwa DNA au vinasaba mwilini.

Saratani huanza wakati sehemu mojawapo ya seli zinapoanza kukua pasipo udhibiti wowote na hivyo kusababisha ukuaji wa seli za saratani kutofautiana na ukuaji wa kawaida wa seli za mwili.

Hali hiyo huchangia kuendelea kukua kwa seli nyingine mpya zisizokuwa za kawaida na baadaye seli hizo za saratani huanza kushambulia ogani nyingine za mwili jambo ambalo halishuhudiwi katika seli za kawaida.

Makundi ambayo yapo katika hatari ya saratani hii.
Ugonjwa wa saratani huweza kumpata mtu yoyote wakati waa maisha yake, lakini kuna makundi ambayo huweza kuwa katika hatari zaidi ya kupata saratani hiyo.

Makundi hayo ni pamoja na watu wenye upungufu wa kinga za mwili, pia wale ambao shughuli zao nyingi hufanyia katika maeneo yenye jua ka muda mrefu na wale wenye tatizo la ulemavu wa ngozi (albino).

Wengine walio katika hatari ya kupata saratani hii ni wale wenye makovu makubwa haya yale yaliyotokana na moto pamoja na wale wenye magonjwa ya ngozi na mabao huzaliwa na uvimbe kwenye ngozi ambao baadaye huweza kubadilika na kuleta saratani.

Mbali na makundi hayo pia inaelezwa kuwa watu wenye ngozi nyepesi mfano wazungu na wenye umri wa zaida ya 60 ndio huwa katika hatari zaidi ya kupata saratani hii duniani kote.

Endelea kuwa karibu na tovuti hii www.dkmandai.com na nitakuletea dalili za saratani ya ngozi.

Karibu Mandai Herbal Clinic kama unasumbuliwa na magonjwa sugu au unahitaji ushauri juu ya masuala mbalimbali ya kiafya. Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic-mhc ili ufikiwe na taarifa zetu kila siku

No comments:

Post a Comment